Mpaka mwaka huu 2018 mkoa pekee usiounganishwa kwa Lami ni Katavi, kwa kumbukumbu za haraka haraka nafikiri Mkoa huu ndiyo wa Mwisho katika nyanja za miundombinu.
Mawasiliano ya barabara kutoka Mpanda/Katavi kwenda Tabora ambapo ni takribani Km 360 inakubidi usafiri siku mbili ulale njiani, barabara ni chafu zimekatika na hakuna kipande chochote cha Lami kwa barabara hiyo.
Halikadhalika kutoka Mpanda/Katavi kwenda Kigoma ni Vumbi/tope japokuwa njia hiyo ina nafuu kidogo.
Ndani ya Mkoa/Wilaya zake ni vumbi lami katikati ya mji haizidi km 25 ni ile ya kutoa vumbi.
Niombeeni nimalize mishe nirudi salama mjini.