Barabara 5 hatari zaidi duniani

Barabara 5 hatari zaidi duniani

Boss Manyota

Member
Joined
Nov 3, 2018
Posts
10
Reaction score
4
Yapo maeneo ambapo barabara ni kizungumkuti na matukio ya ajali ya vifo yamekuwa ya kawaida kabisaaa.

Hizi hapa barabara 5 hatari zaidi duniani.

NAMBA 5
Barabara ya Guoliang kutoka nchini China, hii ni barabara ya chini na inayopita katia miamba na inayotajwa kama miongoni mwa barabara hatari duniani.
Barabara hii ya chini ina urefu wa kilomita 1.2 katika kingo za milima ya Taihang inaupana wa mita 4 na urefu kwenda juu wa barabara hii ni mita tano.

Barabara hii iliyochongwa katika miamba inabaadhi ya kingo zilizo wazi yaani maeneo ya uwazi nah ii imepelekea kupewa jina la utani kama “The road that does not tolerate mistakes” yaani Barabara isiyovumilia makosa.



NAMBA 4 nakupeleka katika Taifa la Pakistan. Hapa unakutana na Barabara ya Karakoram.
Barabara hii ya juu inaunganisha China pamoja na Pakistan kwa upande wa njia ifahamikayo kama Khunjerab katika usawa wa latitudi mita 4,693.

Barabara hii ni maarufu kwa matukio ya kumomonyoka kwa ardhi pamoja na matope na kinachoongeza waasiwasi zaidi ni kuwa barabara hii haijafanyiwa matengenezo yoyote yale.


NAMBA 3
Hapa unakutana na barabara kutoka nchini Iraq,,,hii inafahamika kama Highway of Death yaani barabara ya Kifo.
Barabara hii ilifahamika kama Barabara ya kifo kutokana na historia ya eneo hilo ambapo katika vita vya kwanza vilivyofahamika kama Gulf, msururu wa vifaru vya Iraq na magari ya kivita yalilipuliwa na Marekani mwaka 1991 na kusababisha uharibifu wa magari 2700.
Hivyo basi pembezoni mwa barabara hii kumetapakaa magari chakavu ya kivita pamoja na vifaru jambo ambalo linaifanya kuwa miongoni mwa barabara hatari zaidi na sisizo na usalama duniani.



NAMBA 2

Namaba mbili inashikiliwa na barabara kutoka katika taifa la Bolivia, hii inafahamika kama Road of Death yaani barabara ya kifo.

Barabara hii imewahi kutajwa na shirika la Inter- American Development Bank kama barabara hatari zaidi duniani ambapo katika njia yake kutoka katika mji wa La Paz hadi Coroico unamteremko mkali mno.

Magari makubwa pamoja na mabasi yamekuwa yakijitahidi kupita katika eneo hili lakini yamekuwa yakiiacha njia na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali barabara hii husababisha vifo 200 hadi 300 kwa mwaka.


NAMBA 1 inashikiliwa na barabara kutoka nchini Afghanistan, hii ni barabara ya Jalalabad kuelekea katik mji wa Kabul.

Barabara hii inaurefu wa kilomita 65 kutoka katika mji wa Jalalabad nchini Afghanistan hadi mji wa Kabul ambapo inapita moja kwa moja katika ngome ya magaidi ya Taliban.

Ifahamike kuwa si matukio ya vitisho yanayosababisha barabara hii kuwa nambamoja kati ya barabara hatari zaidi duniani, bali barabara hii ni nyembamba na iliyokuwa na mwinuko unaokwenda juu hadi mita 600 kupitia katika bonde la Kabul.



 
Kuna barabara moja ,ukitokea kwasadala kuingia kijiji cha Uswaa kuna MTO unaitwa "marire" ni Njia hatari sana!
 
Back
Top Bottom