BAO LA MKONO LINAITESA CCM NA SERIKALI YAKE

Kwetu-Tz

Senior Member
Jun 17, 2016
121
101
Heshima yenu wanajukwaa!
Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari yanayoendelea nchini na kugundua mambo mengi na jinsi ambavyo watu mbalimbali kwa kada zao wakijitahidi aidha kukabiliana nayo ama kuyaunga mkono. nasema kukabiliana nayo ama kuyaunga mkono kwani kuna watu wamejitokeza waziwazi bila kupepesa macho kukabiiana nayo huku wengine wakiguna na wengine wakikabiliana nayo kwa kuugulia moyoyoni. Samabamba na hayo kuna wengine wameungana nayo ni sahihi.

Kama nilivyosema katika kichwa cha uzi huu kinachotokea ni MATESO YA GOLI LA MKONO. Wanajamvi sote tunakumbuka August hadi Octoba 2015 msikemshike wa kampeni za uchaguzi makada wa CCM na Makamanda wa UKAWA walivyomenyana katika viwanja mbali mbalimbali vya nchi hii wakijinadi ili wapate ridhaa ya wananchi kiongoza nchi hii. Sisi sote ni mashahidi kwamba kindumbwendumbwe cha kampeni hakikuwa chepesi na ni ukweli usiopingika kwamba ccm ilizidiwa.

Wenye kumbukumbu kama mie hapa mtakumbuka Nape ndiye alisema "tutashinda hata kwa GOLI LA MKONO" Pengine alisema pasipokujua goli la mkono si goli halali na kama alijua basi hakujua matokeo/madhara yake.

sasa nataka kusema kuwa yannayompata yeye ni madhara ya goli la mkono, yanayoipata ccm leo hii ni madhara ya kumpa mtu ushindi wa goli la mkono.

Yumkini si Nape peke yake na CCM bali nawengine kama yule kijana wa pale BUMBULI aliyejifanya msemaji wa chama kwa kipindi hicho. Na ile royal family ya pale Chalinze. Nape my bro usife na Tai shingoni tumeona unavyoeseka step Aside wengine watafuata.

To the poor Innocent Tanzanians, be patient for freedom is coming tomorrow. Things started FALLING APART. Walio juu tutawaona chini na hata kama hatutawaona chini hawafurahii kuwa juu. Majonzi na simanzi vinawaumiza kisa GOLI LA MKONO.

Namaliza kwa kusema hakuna Mkono wa chuma uliotawala ukashinda Nguvu ya UMMA.:(:(
 
Nasikia jeshini wanaandika kwa kalamu nyekundu wakimaanisha kua wapo tayari kufa
 
Back
Top Bottom