Nimefikiria hilo sana lakini naona namna ya uwakilishaji bado haijakidhi alotaka kutuhusisha...
Hapa labda tuchambue kama ifuatavyo, kuna Bao, Kete, Wachezaji wawili.
Bao linatoa fursa ya matundu ili mchezo uchezwe.
Uwepo wa kete unafanya uwepo wa mchezo au hutoa jina la mchezo.
Wqchezaji hawa hutumia nyenzo ya kidole kidondosha kete na vidole kubeba kete.
Moja.
Bao la kete lina matundu mengi, lakini tundu liliwalo ni moja tu.
"Bao la kete" lina tundu moja tu lenye kuhitaji kuliwa.
Mbili.
Bao la kete lina wachezaji wawili ambao wote wana fursa ya kula kete.
"Bao la kete" lina mchezaji mmoja tu mwenye fursa adhimu ya kula kete na amalizapo mchezo(afungapo goli), zigo la kete zake hulibwaga hapo hapo tunduni.
Tatu.
Bao la kete waweza kula mtaji wa mchezaji mwenzako toka tundu lolote utalotulia na kete ya mwisho.
"Bao la kete" halina kula mtaji bali kuliwa mtaji, chovya chovya ya dole tunduni ndio huleta kizaazaa chote hicho cha kubwaga kete zote tunduni na mtaji kuliwa.
Sasa sijui umenielewa? (Kwa sauti ya Kihaya)
mambo ya tafsida hayo kaka. watu na viswahili vyao. mi nimetoka kapa, hasa pale kwenye kula mtaji wa mpinzani duh sijaambulia hata.