Bangi !!

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,515
6,489
Wavuta bangi wawili baada ya kuvuta bangi yao wakawa wanatembea kwenye shamba fulani, wakauona muembe ukiwa na embe linaning`inia, wakaanza kulipopoa na mawe, walifanya hivyo kwa muda mrefu lakini halikuanguka. Baadaye mmoja wao akasema ngoja nipande juu nikalicheki kama limeiva isije ikawa halidondoki kwa vile ni bichi. Alipolifikia embe husika akaliminya na kukuta limeiva. Akashuka chini kwa furaha na kumwambia mwenzie limeiva na tuendelee kulipopoa mpaka lianguke tule!


Source; Mwananchi Jumapili, 20 Nov. 2011.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom