Bandari ya Dar es Salaam ni mlango wa chumbani

Bandari ya Dar es Salaam ni mlango wa chumbani

Fernando Wolle

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
387
Reaction score
772
________________________
Suala la ubinafsishaji wa Bandari ya Dar es Salaam halina tofauti na mikataba ya kina chief Mangungo. Tunaweza kusema tofauti moja tu kwamba Chief Mangungo hakujua kusoma wala kuandika na hakuweza kung’amua kabisa ni nini Dr. Karl Peters alikuwa ameandika na alikusudia kitu gani hasa , alichojali yeye ni kutia dole gumba lake kwenye karatasi na mambo yakaisha lakini viongozi wetu wa sasa wanajua kusoma na kuandika, wanajua nini kimeandikwa na nini kimekusudiwa na kampuni ya DP World lakini kwa kushupaza shingo wanasaini kwa kubebesha msalaba mzito kizazi kujacho cha Kitanzania kisicho na hatia.

BANDARI SALAMA/Bandari ya Dar es Salaam, ni mlango wa chumbani kabisa . Mlango wa chumbani huwezi kumualika mgeni ashirikiane na wewe kuufungua na kuufunga wakati wowote anao taka yeye.

Bandari ya Dar es Salaam na JNIA ni malango makuu ya kuingilia Tanzania kutoka nje ya ardhi ya Tanzania pia ndio kiini cha usalama wa nchi.

Madawa ya kulevya, mali za magendo, vikundi vya kihalifu, makundi ya kigaidi, wahalifu wote kutoka nje ya nchi ni lazima wapitie kwenye milango hii ya nchi.

Kumkaribisha mwekezaji kwenye mlango wa chumbani wa nchi mbali na kunyonywa kiuchumi lakini pia ni kuhatarisha usalama wa nchi.

Kijiografia katika Bara la Africa ni Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pekee ndio unaweza kutoka bahari ya Hindi kwenda Atlantiki na kutoka atlantiki kwenda Bahari Hindi kwa kukatisha nchi mbili tu, kwahiyo hawa waarabu wameona fursa nyingi sana na walikuwa wakimezea mate hii fursa Mungu atusaidie.

Kwahiyo mbali na mkataba wa kinyonyaji pia ushirikiano huu unahatarisha usalama wa nchi kutokana na nature ya mkataba wenyewe.

Ubinafsishwaji wa Bandari ya Dar es Salaam I Unapaswa Kupingwa na yeyote mwenye mwili na akili.

Na linapotokea jambo linalohusu Maslahi ya Taifa tinapaswa kusimama pamoja kwa sauti moja.
 
sasa the way forward ni ipi waarabu hawa wawili Samia na Mbarawa wasiiuze tanganyika. Hili ndilo la kujadili
 
sasa the way forward ni ipi waarabu hawa wawili Samia na Mbarawa wasiiuze tanganyika. Hili ndilo la kujadili
Naona maslahi yenu hayajaziingatiwa ,hii U-turn si ya kawaida,kutoka kusifia mpaka kuponda kwa lugha hizi za kibagudhi si haba
 
Back
Top Bottom