Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,668
Bonge la idea, big up Mpwa
Vipimo vya hilo banda mkuu.
Hello jf mabibi na mabwana natumai ni wazima wa afya baada ya wikiendi.
Ndugu mwanajamii baada ya kuomba ushauri hapa jukwaaa la ujasiriamali, nimeamua kwa ridhaa yangu kuwa mfugaji wa kuku wa kienyeji tiyari nimenunua jogoo(5) na makoo(12) .
Naombeni mnipe ramani ya kuweza kuwalea ktk banda ikizingatiwa baada ya muda mfupi watasaliana kwa wingi.
Muhimu zaidi na banda la vifaranga ambavyo havilelewi na mama yao.
Kadiria tu kutokana na wingi wa kuku wako. Mimi nimejenga 10 kama hilo ambapo kwa kila mita za mraba 9(3X3) wanaingia kuku 100. Hapo kwenye wavu wanashindia ni mita za mraba 15(5X3)
Hongera sana kwa kuingia kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji. Sina ramani ya banda la kuku ila naamini wataalamu hapa watakupatia; nina ushauri tu kwako kuwa ratio ya kawaida ya jogoo kwa mitetea ni 1:10 lakini hapa naona wewe umeanza na ratio ya 1:2.4, nadhani umenunua majogoo wengi sana. Unaweza kuzalisha mayai yasiyo na vifaranga kwa sababu muda mwingi majogoo yatakuwa yakionyeshana ubabe. Hongera sana.
Vizuri mkuu labda kwa mimi ninayeanza unanishauri nijenge la ukubwa gani kwa kuku 15.
hilo eneo la uwazi unaotesha mboga na majani ambayo kuku wanakula. banda nzuri sana
samahani mkuu upo mkoa gani? kam utojali
Mpwa hili banda nimelipenda sana sana, juzi jumamosi nilikua shambani kwangu na ninaanzisha ufugaji wa kuku pia japo mimi nataka nifuge wote wote, nisaidie gharama za jumla kujenga banda moja kama hili lenye uwezo wa kubeba kuku kama mia moja hivi, this is now a Bright Monday.......thanks
Hayo majani yataota saa ngapi wakati kuku watakua wanalittumia?
Ni point nzuri........majani (mchicha) nauotesha katika mabeseni ya plastiki nje ya bandana unapokuwa baada ya kama wiki nawaingizia ndani(unahitaji kuwa na seti mbili ili kukamilisha mzunguko).