kilwakivinje
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 6,003
- 9,095
ANAITWA Peter Banda alipewa ‘Thank you’ yake ndani ya klabu ya Simba. Inanikumbusha namna alivyoingia nchini kwa mbwembwe akipewa jina la ‘Wonder Kid’. Kwamba ni kijana mdogo mwenye maajabu.
Ilinishangaza kuona kijana mdogo wa umri wake anaruhusiwa kutoka Ulaya kuja kucheza Afrika halafu katika nchi ya dunia ya tatu inayoitwa Tanzania. Inatokea nadra kwa vijana wa umri wake kurudi kama wana ubora uwanjani.
Unaweza kukubali kwa mchezaji kama Saido Ntibanzokiza. Kwa mujibu wa Wikipedia inaonyesha kwamba Saido ana miaka 36. Hata kama alidanganya miaka yake lakini haishangazi kuona amerudi tena nyumbani Afrika kumalizia soka lake. Lakini inashangaza kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 22 kama Banda kuja kucheza Tanzania akitokea Ulaya. Hii ilikuwa dalili tosha kwamba hakuwa na ubora huo kama ulivyozungumzwa wakati wa ujio wake.
- Edo Kumwembe. [Mwanaspoti]