Banda hakuwa na uwezo huo kama inavyozungumzwa

kilwakivinje

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
6,002
9,092
ANAITWA Peter Banda alipewa ‘Thank you’ yake ndani ya klabu ya Simba. Inanikumbusha namna alivyoingia nchini kwa mbwembwe akipewa jina la ‘Wonder Kid’. Kwamba ni kijana mdogo mwenye maajabu.

Ilinishangaza kuona kijana mdogo wa umri wake anaruhusiwa kutoka Ulaya kuja kucheza Afrika halafu katika nchi ya dunia ya tatu inayoitwa Tanzania. Inatokea nadra kwa vijana wa umri wake kurudi kama wana ubora uwanjani.

Unaweza kukubali kwa mchezaji kama Saido Ntibanzokiza. Kwa mujibu wa Wikipedia inaonyesha kwamba Saido ana miaka 36. Hata kama alidanganya miaka yake lakini haishangazi kuona amerudi tena nyumbani Afrika kumalizia soka lake. Lakini inashangaza kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 22 kama Banda kuja kucheza Tanzania akitokea Ulaya. Hii ilikuwa dalili tosha kwamba hakuwa na ubora huo kama ulivyozungumzwa wakati wa ujio wake.

- Edo Kumwembe. [Mwanaspoti]
20230906_090440.jpg
 
Banda alikuwa mchezaji mzuri Ila hakupewa nafasi, siku zote alipoingia alibadilisha mpira. Nimeona Mara kadhaa akichezea timu ya taifa Tena kwenye mechi ngumu.
Tatizo kubwa la Simba ni kutaka mafanikio ya haraka badala ya kutengeneza timu ya muda mrefu, Banda, Sakho, Inonga, Kanoute, Phiri ni wachezaji waliotakiwa kukaa pamoja zaidi ya miaka mitatu kutokana na umri wao. Huyo Saidoo anayesifiwa tumemwona mechi zote za kimataifa Hana mchango wowote pia sio mtu anayeweza kuisaidia Simba kimataifa.
Tatizo jingine ni viongozi kuwa na wachezaji wao na pia viongozi wengi was Simba sio mashabiki wa mpira ambao wanafatilia mpira Kila siku.
 
Mchambuzi huyu hapo kashindwa kuweka vema
Kama Banda hakuwa na ubora husika alifikaje Ulaya? Ina maana watu wa Ulaya walinunua mbuzi kwenye gunia?

Ukweli usemwe Banda alinyimwa muda wa kucheza tu nothing more ,na hii ni kawaida hapo Simba , tunakumbatia wachezaji wenye umri mkubwa kuliko wenye umri mdogo.Yupo wapi Rashid Juma?
 
Banda alikuwa mchezaji mzuri Ila hakupewa nafasi, siku zote alipoingia alibadilisha mpira. Nimeona Mara kadhaa akichezea timu ya taifa Tena kwenye mechi ngumu.
Tatizo kubwa la Simba ni kutaka mafanikio ya haraka badala ya kutengeneza timu ya muda mrefu, Banda, Sakho, Inonga, Kanoute, Phiri ni wachezaji waliotakiwa kukaa pamoja zaidi ya miaka mitatu kutokana na umri wao. Huyo Saidoo anayesifiwa tumemwona mechi zote za kimataifa Hana mchango wowote pia sio mtu anayeweza kuisaidia Simba kimataifa.
Tatizo jingine ni viongozi kuwa na wachezaji wao na pia viongozi wengi was Simba sio mashabiki wa mpira ambao wanafatilia mpira Kila siku.
Una upeo mkubwa kama ule wa rafiki yangu Mzee Kilomoni. Yaani umeongea ukweli mtupu.
 
ANAITWA Peter Banda alipewa ‘Thank you’ yake ndani ya klabu ya Simba. Inanikumbusha namna alivyoingia nchini kwa mbwembwe akipewa jina la ‘Wonder Kid’. Kwamba ni kijana mdogo mwenye maajabu.

Ilinishangaza kuona kijana mdogo wa umri wake anaruhusiwa kutoka Ulaya kuja kucheza Afrika halafu katika nchi ya dunia ya tatu inayoitwa Tanzania. Inatokea nadra kwa vijana wa umri wake kurudi kama wana ubora uwanjani.

Unaweza kukubali kwa mchezaji kama Saido Ntibanzokiza. Kwa mujibu wa Wikipedia inaonyesha kwamba Saido ana miaka 36. Hata kama alidanganya miaka yake lakini haishangazi kuona amerudi tena nyumbani Afrika kumalizia soka lake. Lakini inashangaza kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 22 kama Banda kuja kucheza Tanzania akitokea Ulaya. Hii ilikuwa dalili tosha kwamba hakuwa na ubora huo kama ulivyozungumzwa wakati wa ujio wake.

- Edo Kumwembe. [Mwanaspoti]View attachment 2740574
Sawa kwa Simba Ila Sasa huko Ulaya alifikaje nako.
 
Upo sahihi mkuu, najua wengi tu watamtetea ila alikuwa mchezaji wa kawaida wa benchi. Mchezaji mzuri anajipambanua tu haihitaji kubishana. Na hii itatokea pia kwa Dennis Nkane, anaonekana mdogo ila siku zinavyokwenda anaonekana wa kawaida tu.
 
Wachezaji wa Tanzania wana roga sana inawezekana unachosema ikawa kweli ila dogo majeraha yalimrudisha sana nyuma
 
Katika wachezaji mizigo Banda alikuwa wa kwanza Bora ameondoka akaoneshe huo ubora wake. Zaidi ya kukimbia Hana jipya.
 
Ni lini Banda alipewa mda wa kucheza hata mechi tatu mfurulizo ili ahukumiwe?
 
Back
Top Bottom