Balozi Hamisi Kagasheki ashiriki mazishi ya Mama Kabendera

Nakumbuka walivyoteka msiba wa Teja Masogange bila aibu
Siku moja huku kwetu (mikoani) palitokea msiba wa mtu mmoja mwanaccm, yaani nilishangaa jinsi walivyojazana pale, na unajua uzombie walionao, walianza kuonesha uchama, nilitamani kuwafukuza.
 
View attachment 1314435

Kwa Kadri ya macho yangu kuanzia nyumbani, kanisani Chang'ombe hadi kwenye nyumba ya milele Bukoba, huyu ndiye mwana CCM pekee niliyemuona akishiriki msiba huu.

Bila shaka wana CCM wengine walipata udhuru uliosababisha wasionekane na naamini walishiriki msiba huu kiroho na labda waliomba dua za kimya kimya kama desturi zetu zilivyo.

Inshaallah Mwenyezi Mungu azipokee dua zao, Amina.
Huyu mzee ana huruma sana na huwa hapendi dhuluma.
 
View attachment 1314435

Kwa Kadri ya macho yangu kuanzia nyumbani, kanisani Chang'ombe hadi kwenye nyumba ya milele Bukoba, huyu ndiye mwana CCM pekee niliyemuona akishiriki msiba huu.

Bila shaka wana CCM wengine walipata udhuru uliosababisha wasionekane na naamini walishiriki msiba huu kiroho na labda waliomba dua za kimya kimya kama desturi zetu zilivyo.

Inshaallah Mwenyezi Mungu azipokee dua zao, Amina.
Ulikuwa ukiuliza uanachama wa kila m2 aliyehudhuria msibani hapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimewahi kusema humu kuwa viongozi wa ccm na wanachama wao wamekuwa kama Wake wenza was mwenyekigoda mwenyewe.
Kila watendalo kabla wanajiuliza jee atafurahi au atachukia?
Jee wake wenzangu wakiniona watamuambia au watakausha?
Sasa Kabendera amekamatwa na "kuteswa" kwa sababu ya kalamu yake kuandika ubovu wa mwenyekigoda na haya mengine ya DPP anayoshtaki ni funika kombe tuu, sasa kwenda msibani waweza kuhisiwa unaunga mkono aliyo andika Kabendera.
Ni wanaccm kama Kagasheki, Mwandosya,Membe na wengine wachache ndio wana guts za kusimama kwenye ukweli tuu.
Wengine wote kuanzia Dr Bashiru kuja chini ni wake wenza tuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa naonà umeanza kuchanganyikiwa na toka akili zako zote umkabidhi DJ unaandika bila kutumia ubongo. Ulitaka hào wanaCCM wavae kijani ili ujue wameenda wengi?

Leo 7/1/2020 iandikwe kwenye historia ya JF kama siku màda ya kijinga ya Kwanza kutolewa na mwanaJF toka mwaka uanze
 
Naungana mkono na wewe, kuna mdau mmoja hapo chini ame comment kwamba eti 'hii mada ya kijinga ya 2020", naamini katika kukubali ukweli hata kama unauma, ccm ina wachawi wengi sana
 
Jamaa naonà umeanza kuchanganyikiwa na toka akili zako zote umkabidhi DJ unaandika bila kutumia ubongo. Ulitaka hào wanaCCM wavae kijani ili ujue wameenda wengi?

Leo 7/1/2020 iandikwe kwenye historia ya JF kama siku màda ya kijinga ya Kwanza kutolewa na mwanaJF toka mwaka uanze
😆😆😆😆 Sasa mkuu si ungeweka namba ya simu basi ili uonekane upewe japo UDC ! unashindwa hata na Jerry Murro , Mhalifu aliyekamatwa na pingu ?
 
Masaibu ya Erick Kabendera na kifo cha Mama yake vimechukua sana sura ya kisiasa kwa hiyo wanaccm wenye majina makubwa sio rahisi wakaonekana huko vinginevyo yaweza kuwasibu yaliyomkuta Lazarus Nyalandu alipodiriki kwenda kumjulia hali Tundu Lissu akiwa kitandani hospitali ya Nairobi Kenya!
 
Msipowaondoa ccm madarakani mtaendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yenu.
 
Back
Top Bottom