Balile wa gazeti la JAMHURI ni dawa nzuri lakini chungu!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,449
120,805
Nikiwa nawaza ni lini TASNIA nzima ya habari nikimaanisha UANDISHI WA HABARI itapata MAPINDUZI MAKUBWA ya KIUTENDAJI kutokana na UFANISI wake kuwa ni mbovu hasa kutokana na vitendo vya maajabu, vya aibu na ambavyo vingi ni kinyume kabisa na maadili ya UANDISHI WA HABARI hivi karibuni MAKAMU MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ( TEF ) Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Mwalimu, Mwanasheria mtarajiwa na MHARIRI MTENDAJI wa gazeti PENDWA na BORA kwa sasa nchini Tanzania la JAMHURI Bwana Deodis Balile amekuja na UTARATIBU mpya wa KIMAPINDUZI ambao naamini kama USHIRIKIANO ukiwepo basi TASNIA hii ya UANDISHI WA HABARI hapa Tanzania itakuwa na UFANISI mkubwa.

Moja ya MAAMUZI MAZITO KABISA ya KIMAPINDUZI ( ambayo hata hivyo yatawaumiza wale wapenda njia za mkato ambao ndiyo wengi katika tasnia ) yatakayofanyika na ambayo hata Mimi nayaunga mkono yaliyosemwa na Mtu ambaye BINAFSI NAMKUBALI hasa kutokana na kuwa na UWEZO MKUBWA WA AKILI, UCHAMBUZI na MJENGA HOJA mzuri na ambaye kila kukicha ananifanya nizidi KUMKUBALI, KUMUHESHIMU na KUJIFUNZA mengi kutoka kwake ni haya yafuatayo:

· Ifikie UKOMO Watu ambao WANAFELI sana KIDATO CHA NNE au SITA kukimbilia Journalism kama ambavyo ilivyo sasa hapa nchini Tanzania ambapo inasemekana 90% ya WAANDISHI wa HABARI walifeli sana either FORM FOUR or FORM SIX.

· Ifikie UKOMO kwa Watu wanaotoka tu huko watokako na hapa hasa hasa aliwazungumzia WASANII ( wa miziki na michezo ya KUIGIZA ) ambao wengi wao sasa na wao WAMEJIKITA katika masuala ya UTANGAZAJI hasa katika Redio na Tv huku wakiwa hawana hata UJUZI au ELIMU yoyote ya UANDISHI WA HABARI hata tu Basic Course yake ambao wanaharibu kabisa TASNIA nzima na kuifanya ionekane ni ya KIHUNI kitu ambacho kiukweli si ya KIHUNI.

· Kuwa kuanzia sasa kuwepo na CHOMBO MAKINI zaidi akimaanisha kuwepo na BODI MAHSUSI ambayo itakuwa inawapima, kuwachuja na hatimaye kuwapitisha wale ambao kiukweli wanaweza UANDISHI WA HABARI na hapa hasa alikuwa anasisitiza kuwa kutakuwepo na SCHOOL OF JOURNALISM kama ambavyo WAHASIBU wana NBAA na pia WANASHERIA hasa MAWAKILI na wao wana SCHOOL OF LAW ambayo hata kama Wanafunzi wote mlisoma SHERIA lakini baada ya kumaliza masomo yako ili uwe WAKILI basi inakubidi upitie pale SCHOOL OF LAW ukapikwe zaidi na endapo utafeli MITIHANI yao hutoweza kuwa WAKILI na badala yake utabaki tu kuwa MWANASHERIA JOKA LA KIBISA.

· Kuwe na UANGALIZI MKUBWA sana katika hivi VYUO VYA UANDISHI WA HABARI hasa vya NGAZI za chini kama kwa mfano DSJ, TSJ, A3, DACICO, PSJ, RIDER, DAYSTAR, MACMILLAN na vinginevyo ambavyo KIUKWELI imegundulika kuwa hata na vyenyewe ni sehemu ya TATIZO hasa kutokana na kwamba IMEGUNDULIKA kuwa WAKUFUNZI wake wengi hawana SIFA za KUFUNDISHA hali inayopelekea hivyo Vyuo kutoa WAANDISHI WA HABARI WABOVU kama walivyo wao ( WAKUFUNZI wao ) hivyo TEF watakuja na mkazo kuwa hivi Vyuo viajiri WAKUFUNZI ambao ni WABOBEZI katika masuala ya Habari, wamefanya kazi za uandishi wa habari kwa muda mrefu, wanajua changamoto zilizopo, soko lilivyo huko nje na ambao wataweza kuwapa WANAFUNZI wao kile wanachokijua tofauti na sasa ambapo karibia 95% ya WAKUFUNZI / WALIMU ( Tutors ) wa hivi Vyuo hawana UZOEFU wowote KIUTENDAJI wa UANDISHI WA HABARI na wanachokifanya ni KUFUNDISHA tu kile walichojifunza huko Vyuo Vikuu.

· Kuanzia sasa kutakuwepo na KAMATI MAALUM ya kuchunguza MIENENDO hasa NIDHAMU kwa WAANDISHI WA HABARI hasa kutokana na Vitendo vyao vya AJABU, KERO na IABU wanavyovifanya. Mfano WAANDISHI WA HABARI wengi wa sasa huwa wakiitwa tu mahala kwenda kuchukua TAARIFA utakuta wakikaribishwa tu mule ndani wanakosa ustaarabu ambapo wengi wao huomba wapikiwe chai huku wengine wakiiba sukari, vijiko na kama haitoshi hata wakati wa hafla ya chakula WAANDISHI WA HABARI huwa hawasubiri kukaribishwa na badala yake wao HUFAKAMIA tu msosi na kula. Kuna Kiongozi mmoja tena mkubwa tu aliwahi kusema kama ukitaka KUWAUA WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA ANDAA CHAKULA KISHA WAWEKEE SUMU UTAWAUA WOTE akimaanisha kuwa ni WAROHO WA KUTUKUKA. Mfano mwingine utakuta MWANDISHI WA HABARI anaitwa kuchukua Habari lakini anaomba aandaliwe kabisa FUNGU LAKE ( Pesa ) wakati kiuhalisia ni KINYUME kabisa na MAADILI ya Kazi. Mfano wa mwisho utakuta MWANDISHI WA HABARI amesafiri kwenda Mkoa Fulani kuchukua au kutafuta Habari fulani kama za Bunge pale Dodoma utakuta huyo MWANDISHI WA HABARI anaishi kwa kuwategemea tu wale Wabunge kwa kila kitu pale MJENGONI na ipo taarifa moja NYETI kuwa kuna Mtangazaji mmoja alikuwa AKIWAGONGEA SANA WABUNGE PALE KATIKA HOTEL AMBAYO NA YEYE ALIPANGA kuwa wamsaidie na Dawa ya Mswaki kitu ambacho kiliwatia mno wenzake aibu.

Kwako Mtani wangu wa Kihaya Balile na wenzako wote hapa TEF kuwa kama kweli mtayafanyia Kazi haya basi nina uhakika mtairudishia HESHIMA kubwa sana hii TASNIA nzima ambayo Binafsi naona kama vile IMEVAMIWA kama siyo IMEBAKWA na watu ambao kiukweli HAWASTAHILI kuwa WAANDISHI WA HABARI na WAANDISHI WA HABARI WA SASA anzeni KUJICHUJA wenyewe kwani kwa ninavyomjua Balile alivyo MWELEDI WA KUTUKUKA mtapukutishwa wote mwende mkatafute Kazi zingine za kufanya na Mimi namuunga kabisa mkono Balile na TEF kwa 100% juu ya MABADILIKO MAKUBWA WANAYOTAKA kuyafanya kwani TUMECHOSHWA na aina yenu ya UANDISHI, UTANGAZAJI na UPIGAJI PICHA wenu na sasa MTANYOOKA mtake mistake.
 
Hii ni kweli kabisa kuna mtangazaji wa radio fulani anatamka mji wa Cologne kwa kiswahili kama jina lilivyoandikwa.Jamani wapelekwe kupigwa msasa .
 
Hii ni kweli kabisa kuna mtangazaji wa radio fulani anatamka mji wa Cologne kwa kiswahili kama jina lilivyoandikwa.Jamani wapelekwe kupigwa msasa .

Uko Sahihi Na Hongera Kwa Wewe Kuliona Pia Hilo. Hakika WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA Wanahitaji Kupigwa MSASA ULIOTUKUKA Kwani % Kubwa Ni Matatizo, Upuuzi Na Kero Na Ndiyo Wanaoichafua Tasnia Nzima.
 
Hii ni kweli kabisa kuna mtangazaji wa radio fulani anatamka mji wa Cologne kwa kiswahili kama jina lilivyoandikwa.Jamani wapelekwe kupigwa msasa .
Hapa ndipo humkubali masoud masoud wa tbc jamaa jina likiwa la kifaransa basi atalitamka kifaransa hii fani kweli imevamiwa yaani hata kupigwa msasa hawapigwi matokeo yake ndo hayo.
 
Mungu atubariki, atupe nguvu na tuipiganie tasnia yetu isimame kwa miguu yatu hasa katika wakati huu wa majaribu
 
Back
Top Bottom