Balaza La Mawaziri Goigoi: Askofu Mdegela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balaza La Mawaziri Goigoi: Askofu Mdegela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jan 28, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  ASKOFU wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegella (pichani)amedai kuwa utendaji mbovu wa baraza la mawaziri la serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Jakaya Kikwete umekuwa unatokana na mawaziri na viongozi kufanya kazi kwa kutegeana .

  Pamoja na hali hiyo bado amesema kuwa ipo hatari ya maendeleo ya Taifa kuyumba zaidi iwapo chama cha mapinduzi (CCM) kitaendelea kuwepo madarakani na watendaji wa chini kuendelea kumdanganya Rais kwa ajili ya kuonekana wema.

  Dkt Mdegella amesema kuwa ili nchi kurudi katika heshima yake ni vema azimio la Arusha kurudishwa ambalo litasaidia kumaliza ufisadi nchini na kuondoa tofauti ya serikali na mawaziri wake.

  Dkt Mdegella aliyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na gazeti hili kuhusiana na mwenendo wa serikali iliyopo madarakani na sakata la malipo ya dowansi ambayo kwa upande wake amesema kuwa malipo hayo ya dowansi na danganya toto na kuwa serikali italaumiwa zaidi iwapo itakubali kulipa malipo hayo hewa.

  Pia Dkt Mdegella alisema kuwa kasi ndogo ya utendaji kazi kwa baraza la mawaziri umeanza kuwakatisha tamaa wananchi na kuwa ni vema baraza hilo la mawaziri kuongeza kasi zaidi ya utendaji ili kuharakisha kasi ya maendeleo kwa wananchi badala ya mawaziri kuendelea kufanya kazi za chama tawala pekee na kukitetea kwa uovu unaofanyika.

  Hata hivyo alikitaka chama tawala kukaa chini na kukinusuru chama hicho kwa kuwapata wabunge wasema kweli daima ambao watafikisha ukweli wa mambo kwa mwenyekiti wa chama hicho na Rais Kikwete badala ya ilivyosasa kila kiongozi anataka kuonekana mwema kwa Rais na kueleza mazuri pekee na kuacha kufikisha ukweli kwa maana ya hali halisi ya nchi inavyokwenda.

  DKt Mdegella alisema kwa upande wake haweze kutabili kama baraza la mawaziri la sasa litavunjwa ama lah na japo anachokiona sasa ni kushindwa kazi kwa baraza hilo la mawaziri hasa waziri wa nishati ambapo gharama za umeme zimezidi kupaa bila wizara husika kuonyesha uhai wake wa kushusha bei hizo.

  "Mawaziri wengi wa Rais Kikwete wamekuwa wakifanya kazi ya kujipendekeza kwa Rais ....sasa hofu yangu mimi Taifa linaendelea kuyumba ....ila napenda kusema mimi si mtabiri kama Shekh Yahaya ambaye amekuwa akitabili ila naeleza kutokana na uhalisia wa mambo yanavyokwenda sasa

  Alisema kuwa sehemu kubwa ya mawaziri wamekuwa wakionyesha kuogelea katika nafasi zao na kuwa iwapo mambo yataendelea kuwa hivyo nchi inazidi kuyumba zaidi .

  Pia alisema kuwa matamko mbali mbali yanayoendelea kutolewa na CCM kupitia jumuiya zake ni kielelezo tosha kuwa chama hicho kinazidi kufilisika sera na maadili ya CCM ambayo wengi waliyazoea yameonyesha kuyumba zaidi .

  Katika hatua nyingine askofu huyo aliionya serikali kuacha mara moja kuzuia wananchi kufanya maandamano ya kuipongeza ama kuipinga serikali yao kwani kufanya hivyo ni kuzidisha jazba kwa wananchi na kusababisha makubwa zaidi kama ilivyotokea Arusha.


  Source:Mjengwablogspot
   
 2. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ndugu,kila askofu ni shoga? Au huyu specific ni shoga? Acha kuchafua watu wewe. Leta proof,otherwise napendekeza uwe banned kwa kutukana watu.

  MODS: Angalia post ya huyu mtu,si ya kiungwana.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Askofu ni mwananchi kama raia wengine na ana kila haki ya kutoa mawazo yake; haya ni mawazo yake ambayo hakuyatoa kanisani bali nyumbani kwake!
   
 4. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  CCM itawatuma Mashekhe waje kumkemea ASKOFU sasa hivi!!! Anaway, ASKOFU kaongea ukweli mtupu!!!
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ameongea ukweli..
  siku zote ukweli unauma
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono awe banned.
   
 7. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We Bulldozer Huogopi hata Mungu? matusi gani kwa Mtu wa Mungu? kakukosea nini? kama amegusa interest zako si nyamaza kwani lazima useme? sio ustaarabu bwana.
   
 8. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yes, ndo maana tunatakiwa kuona umuhimu wa kumng'oa Kikwete kabla ya 2015. Hii iwe kwa mapinduzi ya kiraia au Kijeshi vinginevyo tubaki kulalamika tu!!!
   
 9. semango

  semango JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Heshima kwako Dr. Mdegella kwa ujasiri na ukweli wako
   
 10. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,861
  Likes Received: 2,786
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini wamemchelewesha huyu mgonjwa huyu!!
   
 11. L

  Leonard Akaro JF Gold Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mheshimiwa utalaumiwa na kila mwanadamu awaye yote yule kumwita Askofu huyu Shoga.
   
Loading...