Balance shobo binti

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
3,019
3,754
Natumai mmeamka salama wadau nataka niwape ujumbe hawa mabinti haswa dada zetu na wengineo wenye jinsia hiyo. Maana imekuwa kiherehere kimewazidi sana kiasi cha kufikia kudandia masuala ya marafiki zao.

Jamani wanawake wenyewe kwa wenyewe huwa hawaaminiani, daima wanakaa na urafiki na mashaka ndani yake. Sasa wewe binti unapokuja kuuliza hali ya uhusiano wa mwenzako kwa mumewe au bwana wake wa kawaida, na akakueleza mbovu kuhusianaa na jamaa yake hadi ukajikuta unamwonea. Licha ya mwanzo ukiwaangalia unawaona kama vile wana furaha, ila unakuja kusikia tofauti.

Ukisikia hayo hebu tuliza makalio yako chini na uachana na masuala ya watu yasiyokuhusu. Mara umshauri avunje uhusiano mara umwandame jamaa yake ili abadilike au amwache mwenzako abaki huru. Au uanze kumfanyia mpango kwa jamaa mwingine unayemwona wewe ni sahihi kama vile unaenda kuishi naye wewe.

Unaambiwa hivyo ili ukae mbali na bwana wake au mumewe usije ukajenga mazoea ya ajabu na ukamzidi kwte. Wanawake wengi husema hilo hata kama ana furaha kubwa na anajihisi alichelewa kumjua huyo jamaa, akihofia ukijua mazuri anayopata utaenda kumzidi kete na kumchukua.

Sasa unasikia hayo na kukimbilia kujifanya mshauri na kununua ugomvi usiyo na maana, mara ugeuke kuwadi kwa jamaa mwingine ili ampate. Binti balance shobo zako, si kila jambo lipo unavyofikiri. Usiharibu furaha ya watu, tafuta jamaa wako akutulize uache kiherehere kama hicho. Na kama una jamaa aongeze juhudi umuwaze yeye tu, uachane na yasiyokuhusu.
 
wilsonwizzo3

JF-Expert Member
May 24, 2018
443
1,779
acha wafu wazike wafu wao

hii week wanaume tumeishi kwa raha sana humu jf
kuna akina dada wametokea kutumwagia sifa kedekede

lakini anakuja mvulana mmoja anajifanya kungwi
mkuu huyo mwanamke aliyeshawishiwa na mwanamke mwenzie ndio anapaswa kulaumiwa,, angekuwa na akili timamu asingeweza kushawishiwa kutafutiwa mwanaume mwingine, nachojua mwanamke mwenye uwezo wa kutafutiwa mwanaume huyo ni mdangaji tu kama sio binti teenager,,
ila unapokuja na bandiko zimazima kutuchambia walimbwende wetu wa jf inakuwa sio sawa kabisa
 
Mr Devil

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
6,825
13,783
Pambana tu na hali yako .mapenzi niya watu wawili na sisi tunao comment apa ni sawa na hao wenye shobo ujue
 
Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
3,019
3,754
acha wafu wazike wafu wao

hii week wanaume tumeishi kwa raha sana humu jf
kuna akina dada wametokea kutumwagia sifa kedekede

lakini anakuja mvulana mmoja anajifanya kungwi
mkuu huyo mwanamke aliyeshawishiwa na mwanamke mwenzie ndio anapaswa kulaumiwa,, angekuwa na akili timamu asingeweza kushawishiwa kutafutiwa mwanaume mwingine, nachojua mwanamke mwenye uwezo wa kutafutiwa mwanaume huyo ni mdangaji tu kama sio binti teenager,,
ila unapokuja na bandiko zimazima kutuchambia walimbwende wetu wa jf inakuwa sio sawa kabisa
Watu wa Twitter ukijikomba kwa kina dada wana msemo huu
IMG_20220617_211828.jpg
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom