Bakwata Dodoma watangaza nafasi zinazogombaniwa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,102
114,701
BARAZA Kuu la Waislamu
(BAKWATA), Mkoa wa Dodoma
limewataka waislamu kujitokeza
kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi katika Baraza hilo.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari,
Ofisini kwake, Mjini hapa
jana, Katibu wa Baraza
hilo Mashaka Kitundu,
amesema Baraza hilo
limetoa fomu za
kugombea nafasi
mbalimbali.
Kitundu, alizitaja nafasi
zinazogombaniwa kuwa ni
Baraza la Masheikh Mkoa watu 5,
Halmashauri Kuu Bakwata Mkoa
nafasi 10 na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu Taifa nafasi
moja.
?Katika hii nafasi ya Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa
tumetoa fomu kwa sababu
nafasi imebaki wazi kutokana na
aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo
kufariki dunia,?? amesema
Kitundu.
Kitundu, amesema baada ya
kupatikana wagombea hao,
majina yao yatapelekwa kwenye
Baraza Kuu la Ulamaa kwa ajili ya
kufanyiwa usaili na baada ya
usaili huo yatarejeshwa mkoani
hapa kwa hatua nyingine.
Aidha, Kitundu amewataka
waislamu kujitokeza kwa wingi
katika kugombea nafasi hizo,
kwani kwa kufanya hivyo
kutasaidia katika kujenga umoja
ambao ni muhimu kwa Waislam
 
Kwa mfumo huo wa katiba ya bakwata kama ya ccm,tusitegemee mabadiliko kamwe.mimi nilidhani nafasi za Mkurugenzi Mkuu,Fedha na Utawala,Elimu,Uwekezaji,Huduma za jamii etc yaani kuwe na (Trustee na Management)
 
Wabadili katiba iruhusu hata tusio na dini ila tuna taaluma na uwezo wa kuiendeleza bakwata hasa idara zinazohitaji taaluma kama kitengo cha fedha,rasilimali watu nk.
 
Back
Top Bottom