Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Mzungu mmoja aliwahi kunikebehi akasema sisi Waafrika kwy Kiswahili tunamuita mtu toka nchi za Magharibi Mzungu, akaniambia ebu sasa ondoa herufi z kwenye neno Mzungu alafu ulisome.
Akajinasibu kwamba Mzungu ni mungu wa weusi ndiyo maana tunawategemea kwa kila kitu hata kibovu, yakiwemo mawazo.
Bakita badilini huu msamiati dhalili kwetu. Hautufai. Kiswahili ni tajiri wa misamiati tutafutieni mwingine.
Vinginevyo tukusanye saini za watu tukaiombe Mahakama iufute toka kwenye matumizi.
Lakini mjuwe kama hamjaandaa msamiati mbadala patakuwa na ombwe endapo Mahakama itachukuwa hatua mapema.
Aidha, sina hakika aliyebuni msamiati huu ni nani hasa na kama hakupewa chochote kitu na hawa miungu mieupe ya Afrika!
Nawasilisha.