Bajeti ya Magufuli Sh1 trilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Magufuli Sh1 trilioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by baraka moze, Jun 6, 2012.

 1. b

  baraka moze Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwandishi Wetu
  KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imeipitisha bajeti ya Wizara ya Miundombinu, ambayo ni Sh1,023,033,626,000.

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alisema kipaumbele cha wizara katika bajeti hiyo ni kuhakikisha barabara zote nchini zinaunganishwa kwa kiwango cha lami. Juzi, Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa, alisema bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13 inatarajiwa kuwa Sh15 trilioni katika vipaumbele saba.

  Bajeti inayomalizika ilikuwa Sh13.5 trilioni.
  Serukamba alisema katika miradi ya maendeleo, fedha za ndani ni Sh296,896,892,000 na fedha za nje ni Sh397,051,380,000 na kwamba, jumla ni Sh693,948,272,000.

  "Mishahara ya wizara na taasisi ni Sh21,340,508,000, mfuko wa barabara Sh300,764,800,000, matumizi mengine ni Sh6,980,046,000 na jumla yake ni Sh329,085,354,000," alisema Serukamba.

  Alisema bajeti hiyo imepita kwa urahisi kwa sababu fedha nyingi zimepelekwa katika miradi ya maendeleo.

  "Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya kulipa madeni yote ya wizara ambayo mpaka mwishoni mwa Juni mwaka huu yatakuwa yamelipwa. Ila tumewataka kuhakikisha msongamano wa magari Mwanza, Dar es Salaam na Arusha unakwishwa," alisema Serukamba.

  Alisema barabara zote za Dar es Salaam zimechukuliwa na Wakala wa Barabara (Tanroads) na zitajengwa kwa kiwango cha lami.
  Vipaumbele katika bajeti hiyo ni miundombinu ambayo ina vipengele vinne; umeme, usafirishaji na uchukuzi, mawasiliano na maji salama.

  Vipaumbele vingine ni kilimo, viwanda, rasilimali watu na huduma za jamii, utalii, biashara za ndani na n je na huduma za fedha


  Source: Mwananchi ya tarehe 05 June 2012 19:19
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sounds gud to me, pesa nyingi kwenye maendeleo leo expenditure za kawaida.
   
 3. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Je zitawafikia walalahoi?
   
 4. b

  baraka moze Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hizo ni neema za watu sasa tusubiri utekelezaji:glasses-nerdy:
   
 5. v

  victor11 Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sound good, but funds need to disbursed on time, budget displine is foundamental in achieving expected objectives.
   
 6. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ni njema iwapo mipango itatekelezeka.
   
Loading...