kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
IDADI ya watu wanaopata majisafi na salama imeongezeka na kufikia asilimia 72 ya wakazi wa vijijini na asilimia 86 kwa mijini huku Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ikiongezeka kwa asilimia 77.01 kwa mwaka 2016/17. Katika bajeti iliyowasilishwa jana bungeni mjini hapa, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge analiomba Bunge liidhinishe Sh 939,631,302,771.
Kati ya fedha hizo, matumizi ya kawaida ni Sh 24,437,365,000, ambapo Sh 7,075,948,000 sawa na asilimia 28.96 ni kwa ajili ya kugharimia Matumizi Mengineyo (OC) na Sh 17,361,417,000 sawa na asilimia 71.04 ni kwa kulipa mishahara. “Jumla ya Bajeti ya Maendeleo ni Sh 915,193,937,771 ambazo kati ya hizo Sh 690,155,000,000 sawa na asilimia 75.41 ni fedha za ndani na Shilingi 225,038,937,771 sawa na asilimia 24.59 ni fedha za nje,” alisema Lwenge.
Kwa mujibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mifugo, Kilimo na Maji, ongezeko hilo la bajeti ni asilimia 77.01 wakati bajeti ya maendeleo imeongezeka kwa asilimia 81. Mwaka 2015/16, wizara hiyo iliidhinishiwa Sh 458,900,981,000. Akiwasilisha hotuba yake, Lwenge alisema hadi kufikia Machi, 2016, jumla ya watu 21,907,506 waishio vijijini wanapata huduma ya majisafi sawa na asilimia 72 ya wakazi waishio vijijini.
“Idadi ya watu wanaopata huduma ya maji vijijini imeongezeka kutoka milioni 15.2 sawa na asilimia 40 ya wananchi wanaoishi vijijini mwezi Julai, 2013 tulipoanza utekelezaji wa BRN kufikia watu milioni 21.9 sawa na asilimia 72 mwezi Machi, 2016,” alisema.
Lwenge alisema katika Awamu ya Pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji, serikali imepanga kujenga miradi mipya ya maji vijijini katika vijiji 2,052 itakayokuwa na vituo vya kuchotea maji 38,549, kukarabati miradi ya maji katika vijiji 1,107 yenye vituo vya kuchotea maji 19,889. Vingine ni pamoja na kupanua miundombinu ya maji katika vijiji 946 itakayokuwa na vituo vya kuchotea maji 17,852.
“Jumla ya wananchi wapatao 19,080,000 waishio vijijini wanatarajiwa kupata huduma ya maji. Lengo la serikali ni kuhakikisha ifikapo mwezi Juni, 2020 asilimia 85 ya watu waishio vijijini wanapata huduma ya maji,” alisema Waziri. Alisema kwa mwaka 2016/17, kiasi cha Sh bilioni 463.30 (Sh bilioni 373.34 za ndani na Sh bilioni 89.96 za nje) zimepangwa kutumika kutekeleza miradi ya maji katika vijiji 786 kwa kujenga vituo 14,031 vya kuchotea maji na wakazi wapatao 3,520,250 waishio vijijini watanufaika na maji.
Akizungumzia maji mijini alisema kwa upande wa miji mikuu ya mikoa, upatikanaji wa huduma ya maji uliongezeka kutoka asilimia 80 mwaka 2007 hadi asilimia 86 mwaka 2015. Waziri Lwenge alisema kwa Jiji la Dar es Salaam umeongezeka kutoka asilimia 55 hadi 72 na asilimia 41 hadi asilimia 60 kwa Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa.
“Katika mwaka 2016/17, wizara imetenga jumla ya shilingi bilioni 392.4 fedha za maendeleo kwa ajili ya miradi ya maji mijini. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 240 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 152.4 ni fedha za nje,” alisema Lwenge. Aidha alisema serikali itaendelea kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika miji mikuu ya wilaya na miji midogo kwa kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi katika miji hiyo.
Imetenga Sh bilioni 17.4 kutekeleza kazi hiyo. Alisema pia Wizara itaendelea kuzijengea uwezo Mamlaka za Maji Mijini ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo yanayohudumia, hatimaye zijiendeshe kibiashara na kuwahudumia wananchi kwa ufanisi. Akizungumzia miradi ya kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka miji mbalimbali, alisema usanifu wa mradi huo utakamilika Juni mwaka huu, na katika mwaka 2016/17 wizara itaanza ujenzi wa mradi huo utakaogharimu Euro milioni 313.
Kuhusu uwezo wa taasisi za wizara hiyo, alisema hadi kufikia Machi, 2016 kuna jumla ya wataalamu 2,224 katika ngazi ya Wizara, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya, na hivyo sekta kukabiliwa na upungufu wa wataalamu wapatao 9,924. Alisema upungufu huo unatokana na watumishi kustaafu, kufariki au kuacha kazi, serikali kutoajiri kwa muda mrefu pamoja na kuongezeka kwa idadi ya mikoa na halmashauri.
“Wizara inaendelea na majadiliano na mamlaka zinazohusika na ajira serikalini ili kupata ufumbuzi wa kuziba nafasi za wataalamu ambazo ziko wazi,” alieleza Lwenge kuhusu kukabili tatizo hilo. Kuhusu sekta ya umwagiliaji nchini, alisema nchi ina jumla ya eneo la hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa umwagiliaji. “Hadi sasa, eneo linalomwagiliwa ni hekta 461,326 sawa na asilimia 1.6 ya eneo lote linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na linachangia asilimia 24 ya matumizi yote ya chakula nchini kwa sasa,” alisema.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Mifugo, Kilimo na Maji, Makamu Mwenyekiti wake, Dk Christine Ishengoma alipongeza vipaumbele vilivyotengewa fedha za miradi ya maendeleo. Hata hivyo, aliishauri Serikali kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vinatolewa kama zilivyoombwa kwa wakati, kwani katika bajeti inayomalizika, fedha zilitolewa ni kidogo hivyo kukwamisha miradi ya maendeleo.