Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Kilimo bado ndiyo sekta muhimu katika uchumi na maendeleo kikiwa kimeajiri asilimia 75 ya Watanzania na kinachangia zaidi ya asilimia 100 ya chakula kinachopatikana nchini kwa miaka yenye mvua za kutosha.
Aidha, kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, katika mwaka 2015 Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29.0 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na asilimia 28.9 mwaka 2014 ingawa ukuaji wa sekta hiyo uliporomoka kufikisa asilimia 2.3 ikilinganishwa na mwaka 2014 ambapo ukuaji ulikuwa asilimia 3.4.
Kwa mwaka 2014 uzalishaji kwa kilimo cha umwagiliaji ulikuwa tani 3,141,237.34 sawa na asilimia 24.6 ya mahitaji ya chakula nchini wakati ambapo uzaliashaji wa mazao ya bustani umeongezeka kutoka tani 5,635,364 mwaka 2014/2015 hadi tani 5,931,906 mwaka 2015/2016.
Kwa habari zaidi, soma hapa=> Bajeti ya kutosha katika umwagiliaji itasaidia kuondoa njaa nchini | Fikra Pevu