Bajeti ya 2017/18 kuwa shilingi trilioni 31.7

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Habari wadau,!

Bajeti ya mwaka 2016/2017 ilikuwa takribani Tril 29 na makusanyo yetu kwa mwezi ni wastani wa tshs 1.2 ambayo kwa miezi 12 yaani July mwaka 2016 hadi June 2017 ni kama trilioni 15. Kilichosalia ni misaada na mikopo toka nchi wahisani.

Na kwa mwaka huo wa fedha inajulikana wazi kabisa wahisani wameyeyuka kwa sababu zao wanazozijua na baadhi sie tunazijua.

Habari zilizopo ni kuwa kwa mwaka ujao wa fedha 2017/2018 bajeti itapanda hadi kufikia trilioni 32 hadi 33.

Najiuliza kwanini tuandike au kukadilia fedha nyingi kuliko uwezo wetu na kujipa matumaini hewa?

Chanzo kikubwa cha mapato ni vinywaji na mwaka huu mmetia hasara kwa wafanya biashara zaidi ya trilioni 2.Wafanyakazi wanaotoa kodi kihalali ndio hao mliowapiga asilimia 15 ya bodi.

Na juzi waziri katangaza hakuna kupanda daraja au cheo bila kupitia kozi maalum hii ina maana hakuna mshahara mpya.

Taarifa ya IMF inasema hakuna gorvenment expenditure ina maana hakuna mzunguko wa fedha. Means hata wale wafanyabiashara wadogo wanaisoma namba.

Hakuna projects mpya zakuongeza mzunguko hasa private sector ndio hao mnaosema wajiajiri wakati serikali yako inasema vitu vyote vifanywe na serikali.

Hiyo kodi itatoka wapi?
 
Mwaka jana tulijidanganya na mwaka huu tunajidanganya zaidi.
Tunapanga namba nyingi wakati mwaka jana wizara na halmashauri zinalalamika kutopokea mafungu ya bajeti zao
 
Mwaka jana tulijidanganya na mwaka huu tunajidanganya zaidi.
Tunapanga namba nyingi wakati mwaka jana wizara na halmashauri zinalalamika kutopokea mafungu ya bajeti zao

Na kinachoshangaza ni bajeti ya maendeleo inazidi kupigwa panga. Matumizi yanakua mengi uku akijinasibu anabana matumizi.
 
hizo figure ni siasa tu. Kwenye halmashauri zetu hata 20% ya bajeti haijafika na ni almost kila mwaka!

Muhimbili tu juzi niliona wanalia hawajapewa 3bln zao na imebaki miezimitatu tu bajeti iwe imeeksipaya,naibu waziri wa Afya akasema wavutr subira hali ngumu!
 
Kupanga ni kuchagua lakini sina uhakika kama kuchagua ni kupanga
 
Wanasema(ga) namba hazidanganyi.....hivyo ni mwendo wa namba tu hata kama hakuna uhalisia. Kimsingi kila hatua huanza na moja kwa urahisi, kama hiyo moja(0.......1) tumeshindwa kuikamilisha, ni vipi tuizungumzie 100?

Kama tuna uwezo wa kukusanya trilioni 15 kwa mwaka, matumizi yetu yapangwe na kuishia hapo tu, si ndo uwezo wetu?!!! Tukipata ziada(misaada), iwe iliyotarajiwa au haikutarajiwa, iingie kwenye shughuli ambazo haziko kwenye utekelezaji wa bajeti yetu.

Kinyume na hapo, kila siku tutaendelea kudanganywa na wasomi kuwa uchumi umekuwa kwa asilimia 7 huku wakirudia chorus yao ya NAMBA HAZIDANGANYI, ukibisha kidogo watakwambia ufatilii mambo, hata USA iko hivyo Na hivi hizo saba tangu zimeanza kutajwa zimeshafika ngapi???
 
bajeti inapitishwa lakini haifiki kule ilikokusudiwa,je kwa nini wapange na watu walopangiwa wasipewe haki yao
 
Bajeti ya kwenye makaratasi, kuna wizara/project zinapangiwa bajeti lakini fedha hamna. Sasa kwa nn tujidanganye kwenye makaratasi wakati uhalisia tunaujua?
 
Haya ni mazingaombwe. Hii nchi inaendeshwa kwa kiki. Viongoz wanagombea front page ili wauze.
Ngoja tuone km walishindwa kununua mbuzi ng'ombe wataweza?
 
Hamna lolote hapo,tushazoea bajeti zisizotekelezeka tena ya JPM ndo kabisaa..... Itaendelea kuwa changa la macho tu. Muulizeni GAG,nafikiri report ya budget kwa mwaka wa fedha unaokwisha haitaandikika!!
 
Mpaka sasa wametoa kiasi kiasi gani katika zile billion 250 za madawa kwa Wizara ya Afya?
 
hii nchi tajiri sana according to Magufuli,hiyo bajeti ndogo sana tusimpangie,alichukua fomu mwenyewe msimpangie bajeti.
 
Back
Top Bottom