Bajeti ya 2017/18 kuwa shilingi trilioni 31.7

Bajeti ya kipumbavuuuuu!! Iliyopita yenyewe haijatoka hata 30%! Hivi kuna ubaya gani kutoa realistic budget? Kwa mfano makusanyo yetu kama ni 14 trillion tukazigawa hizo hizo kwa shughuli zetu? Lenye bichwa kama embe dodo la Tanga ndo litabaki kutupiga vijembe utafikri limefanikiwa mno! Wabunge msaidieni Rais kupanga bajeti halisi ili tuache maigizo au mnaogopa mtatumbuliwa?
 
  • Thanks
Reactions: 314
Mpaka sasa hivi makusanyo ya kodi ni 0.0001%,maana unalipa kodi wakati hakuna biashara?Akina GSM wanawalipa wale wanaoitwa Almasi kwa kiinglish halafu hawalipi kodi yaani kodi ni 0 halafu unategemea kupata pesa,mkikosana ndipo mnaissue tax invoice.Kazi kweli kweli
 
Bajeti ya kipumbavuuuuu!! Iliyopita yenyewe haijatoka hata 30%! Hivi kuna ubaya gani kutoa realistic budget? Kwa mfano makusanyo yetu kama ni 14 trillion tukazigawa hizo hizo kwa shughuli zetu? Lenye bichwa kama embe dodo la Tanga ndo litabaki kutupiga vijembe utafikri limefanikiwa mno! Wabunge msaidieni Rais kupanga bajeti halisi ili tuache maigizo au mnaogopa mtatumbuliwa?
Mkuu punguza hasira utatolewa bastora
 
Habari wadau,!

Bajeti ya mwaka 2016/2017 ilikuwa takribani Tril 29 na makusanyo yetu kwa mwezi ni wastani wa tshs 1.2 ambayo kwa miezi 12 yaani July mwaka 2016 hadi June 2017 ni kama trilioni 15. Kilichosalia ni misaada na mikopo toka nchi wahisani.

Na kwa mwaka huo wa fedha inajulikana wazi kabisa wahisani wameyeyuka kwa sababu zao wanazozijua na baadhi sie tunazijua.

Habari zilizopo ni kuwa kwa mwaka ujao wa fedha 2017/2018 bajeti itapanda hadi kufikia trilioni 32 hadi 33.

Najiuliza kwanini tuandike au kukadilia fedha nyingi kuliko uwezo wetu na kujipa matumaini hewa?

Chanzo kikubwa cha mapato ni vinywaji na mwaka huu mmetia hasara kwa wafanya biashara zaidi ya trilioni 2.Wafanyakazi wanaotoa kodi kihalali ndio hao mliowapiga asilimia 15 ya bodi.

Na juzi waziri katangaza hakuna kupanda daraja au cheo bila kupitia kozi maalum hii ina maana hakuna mshahara mpya.

Taarifa ya IMF inasema hakuna gorvenment expenditure ina maana hakuna mzunguko wa fedha. Means hata wale wafanyabiashara wadogo wanaisoma namba.

Hakuna projects mpya zakuongeza mzunguko hasa private sector ndio hao mnaosema wajiajiri wakati serikali yako inasema vitu vyote vifanywe na serikali.

Hiyo kodi itatoka wapi?
Bajeti ya mwaka 2016/2017 ilikuwa trilion 29- je tulitimiza kwa kiasi gani? Projection ya TRA ilikuwa kukusanya shilingi ngapi na walikusanya ngapi
 
Mpango ni wakupanguliwa mwaka jana hawajaweza hata kufikia 50% mobilization za resources kwa ajili ya kutimiza bajeti waliyoipachika ya 2016/17 leo hii anakuja na kichekesho kingine they love numbers but numbers dont lie pole serikali ya mapedeshee, matapeli mambumbu watu muliokosa vision mumeuwaa vyanzo vyote vya kuingiza mapato sasa hivi hata monthly corrected revenue you never make it open to the public mazero hamjiwezi achieni nchi wenzenu wawafundishe
 
Nimesoma mawasilisho ya waziri wa Fedha na Mipango kuwa tutakusanya 31:6 Trilioni kutoka tulizoshindwa kupata 29:5 Trilioni.Mojaya sababuza kushindwa
kufikia makusanyo ya 2016/17 ni ukweli mazingira ya wafanyabiashara nchini ni magumu mnoo na sababu za nje ni kupingana na dhana ya kimataifa ya utawala bora.tunaonekana kama sio taifa linaloaminika kukopesheka na kwa wawekezaji kuweka mitaji yao hapa nchini.

Cha kufanya tuwe na mipango inayotekelezeka na kusimamia sheria na utawala bora wa kufuata sheria ili kurudisha imani ya wawekezeji wa nje na wa ndani pia na wakopeshaji.pia kuachana na dhana ya kutegemea mapato mengi kutoka kwa wananchi huku matumizi ya serikali yakibanwa.Mpaka sasa asilimia 34 hela za maendeleo zimetolewa bado miezi minne mda wa bajeti uishi.huku matumizi ya kawaida ya idara na wizara za serikaki wakiwa hoii!
 
Serikali imewasilisha makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka 2017/2018 kiasi cha Trilion 31.6.

Hii ni budget mpya na kubwa huku Budget ya mwaka jana (ndogo) ya Trilion 29.57 ikiwa imeshindwa kutekelezwa. Mf. Pesa za miradi ya maendeleo Trilion 11 (100%)ni Trilion 3.9 tu(34%) ndizo serikali iliweza kuzitoa mwaka jana. Moja ya sababu kubwa ni misaada kutoka kwa wahisani kupungua kutoka Trilions to Billions. Mf. Ni MCC, nk.

Mm napendekeza VIWANJA VYA Michezo/MPIRA TZ vyote; Mf. Shekh Amri Abeid- Arusha. Uwanja wa Karume -Musoma, CCM KIRUMBA -Mwz, nk vitaifishwe na viingie serikali kuu na kuendeshwa ki biashara zaidi.

Hivi viwanja vilijengwa chini ya chama kimoja TANU na ilikuwa lazima kwa kila mtumishi kujiunga na TANU, upenda au usipende. Pia viwanja hivi vilijengwa na wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kwa kuchangia nguvu. Mf. Kufyatua tofali, kusomba mawe, kuchota maji, kusogeza mchanga, nk. Hii ilikuwa lazima siyo ombi.

Baada ya TANU kuvunjwa na kuzaliwa CCM. Na baada ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ingelikuwa bora iwapo mali za umma (wananchi wote) ingekabidhiwa serikali na mali za vyama kutenganishwa. Ni maajabu Tz mali za umiliki wa raia wote kuitwa mali za CCM baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992.

Hizi pesa CCM wamekuwa wakilipana Posho na zingine kuishia kupigwa kiaina. Ni bora zitumike kuleta maendeleo kwa wote ktk miradi ya maji, umeme, nk.

Rais ushauri ni mhimu kwa nchi yetu na kwa hulka yako ungependa kuona Tz tukijitegemea.
Kama ww ni mzalendo wa Kweli fanya hili jambo kwa maslahi ya Taifa.

Wadau mnakaribishwa kujadili hili suala na kuchangia vyanzo mbadala vya mapato kwa serikali yetu.
 
Hela za kuwalipa watu wa mtandaoni unafikiri watazitoa wapi? wakina lizabon unataka waone Lumumba pachungu?
 
ukitaka hizo mali ziwe zako, yaani na wewe uwe mmoja wa wamiliki, chukua kadi ya ccm tu. simple wala usianze kuzunguka sana. hutaki kaa kimya. mwanamke akiamua kwenda kwa hiari yake bila kufukuzwa na mumewe hana haki ya kudai mali waliochuma na mmumewe. akitaka kuzitumia arudi nyumbani.
 
Haya yalishatarajiwa kitambo sana kilichobaki kwa Sizonje Supporters ni ku-swallow their pride manake walifikia kuota kukusanya trillion 8 kwa mwezi matokeo yake tunaenda mwaka wa pili sasa hata 1.2 haipatikani!!!
 
Na kinachoshangaza ni bajeti ya maendeleo inazidi kupigwa panga. Matumizi yanakua mengi uku akijinasibu anabana matumizi.
Sioni hata maana ya wabunge kwenda Dodoma kwa ajili ya bajeti maana tumeona Boss akipanga mwenyewe kutokea mjengoni.
 
Nini maoni kwa machungu uliyoyaonja kwa kutotekelezeka Bajeti inayoishia, halafu zimeongezeka tarakimu lukuki kwenye bajeti ijayo!
 
Nini kilichokwamisha kufanikiwa na kusifiwa kwa Bajeti ya kwanza ya 'HAPA KAZI TU'? Maana fedha zilizopangwa kwenda hazikwenda; zilizopangwa kupatikana hazikupatikana; zilizopangwa kubaki hazikubaki. Mambo yakawa tofauti. Bajeti ya 'HAPA KAZI TU' imeandika historia ya 'kuboronga' kuliko zote (kwa mujibu wa Tundu Lissu).

Ziara za bandarini, TRA, makusanyo ya kutosha na kutisha ya Polisi,mirabaha ya madini,wahisani na kadhalika yamekumbwa na 'kidudumtu' gani? Nani kakwamisha Bajeti ya kwanza na ya mfano ya 'HAPA KAZI TU'? Hicho kidudumtu tunakidhibitije kama nchi na kung'arisha utawala huu wa 'HAPA KAZI TU' na nchi yetu kwa ujumla?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Dkt Bashiru Amesema ni mapema kuchangia kabla ya kuisoma
Watu wameanza kupinga bila hata kusoma
 
Back
Top Bottom