Bajeti ya 2016/17, TZS 3.1 Mill tu ndo zilizotoka kati ya TZS 11.8 Mil zilizopitishwa na Bunge

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango, katika kuwasilisha Makadirio Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 yalikuwa ni sh trillion 29, Mwaka huu Serikali inatarajia kuongeza bajeti kwa Trillion 3, kufikia trilion 32 kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Leo hii mjini Dodoma Dr. Philip Mpango amesema kuwa Fedha za Miradi ya Maendeleo katika bajeti inayoishia 2016/2017 Kati ya Sh11.8 trilioni zilizopendekezwa katika bajeti hiyo, zimetolewa Sh3.1 trilioni pekee (asilimia 34) kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Nini Maoni yako!?
Nakutakia Tafakari njema.
 
lakini bado 4 months...so bado tunamda
 
Pia weka na sababu alizotoa kwanini hazikutolewa zote???

Ili tuweze kuainisha vizuri....
 
Kwa maana hiyo katika bajeti ya 2016/2017 mwaka wa fedha ni 34% ndiyo iliyotekelezeka na 66% hakuna kitu. Tuliaminishwa kuwa katika kufinya na kubana matumizi yasiyokuwa na ulazima ili hizo fedha zipelekwe kwenye maendeleo kumbe nako ilikuwa na kutudanganya kwenye makaratasi. Tena wakatoka vifua mbele bajeti ya kumkomboa masikini, kumbe ndiyo angamizo kwa masikini kwa kumnyanganya ata kile kidogo alichokuwa nacho.

Wanapanga nakisi ya bajeti isiyotekelezeka na mipamgo lukuki hawajui ata waanzie wapi, washike lipi na kuacha lipi. Ni kama tunajiendea kwa matamko tu. Tena sidhani kama kuna umuhimu wa bunge kama kuna mtu mmoja anajiona kila kitu ndiyo yeye tu na kujipangania bajeti na kutekeleza mwenyewe.
 
Hivi matumizi yalofanyika(ununuzi wa panga bai) hiwezi kua walichota humo ndo maana hazijatosha,coz bunge halikupitisha kweny wizara husika.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango, katika kuwasilisha Makadirio Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 yalikuwa ni sh trillion 29, Mwaka huu Serikali inatarajia kuongeza bajeti kwa Trillion 3, kufikia trilion 32 kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Leo hii mjini Dodoma Dr. Philip Mpango amesema kuwa Fedha za Miradi ya Maendeleo katika bajeti inayoishia 2016/2017 Kati ya Sh11.8 trilioni zilizopendekezwa katika bajeti hiyo, zimetolewa Sh3.1 trilioni pekee (asilimia 34) kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Nini Maoni yako!?
Nakutakia Tafakari njema.
jamani hivi ni mimi peke yangu au? mbona 3.1 tr ni 26% ya 11.8 tr? 34% inatoka wapi?
 
Budget inayoishia mwezi June ni Sanaa tupu... Hata km ni tafiti halafu hypothesis yako imeleta majibu ya 34%,hiyo ni null!!!!!! Hawa vingozi wetu sijui wokoje, wanafikiri kwamba watanzania wote ni mafala eti wakati wao ndo zaidi..
 
Back
Top Bottom