Bajaji yangu nimeipata lakini imechakaa sana

iamriq_arthur

JF-Expert Member
May 1, 2021
377
884
Guys, hivi juzi nilikuja na uzi wa kuibiwa bajaj yangu, leo bajaj nmeipata baada ya kumpeleka mdhamini mahakamani na mwizi wa bajaj akaamua kuitelekeza mahala na kupiga simu akatoa location sehemu alipoiacha bajaj, nimefatilia sehemu hiyo mpaka kufika, nimekuta bajaj imeshachakaa sana, imeshakua mbovu na haiwaki.

Inshort ni kuwa inahitaji service ya hali ya juu sana mpaka iweze kurudi kwenye uhafadhari.

Naombeni ushauri wenu, niendelee kudeal na mdhamini wake ambae ni mama yake ili aweze kugharamia service ya hii bajaj.? Ama nifanye nini?

=========
Soma Pia: Naipataje Bajaj yangu iliyoibiwa
 
Daah Ila madogo wanazingua sana, unampa chombo hajui umejidhiki kiasi gani, m9 si mchezo, afu mwisho wa siku anakuletea uhanithi.

haki vile pesa inauma, kama vipi deal na huyohuyo bimkubwa auze hata kiwanja cha urithi aitengeneze.
Sometimes inabidi uwe bandidu ili ufanikiwe.
 
Natamani kujua alimthamini Kwa maneno TU au rehani, ila toto lililoshindikana Kwa mzazi ndio wewe umewekeza!? Pole sana
 
Guys, hivi juzi nilikuja na uzi wa kuibiwa bajaj yangu, leo bajaj nmeipata baada ya kumpeleka mdhamini mahakamani na mwizi wa bajaj akaamua kuitelekeza mahala na kupiga simu akatoa location sehemu alipoiacha bajaj, nimefatilia sehemu hiyo mpaka kufika, nimekuta bajaj imeshachakaa sana, imeshakua mbovu na haiwaki.

Inshort ni kuwa inahitaji service ya hali ya juu sana mpaka iweze kurudi kwenye uhafadhari.

Naombeni ushauri wenu, niendelee kudeal na mdhamini wake ambae ni mama yake ili aweze kugharamia service ya hii bajaj.? Ama nifanye nini?
Kwa vyovyote vile inabidi ulipwe ama una wazo mbadala? Ingia naye makubaliano ya kuigharamikia.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mshikilie mamaake acha huruma utakufa maskini, ukiendelea kideal na mama watajitokeza tu
 
Shukuru Mungu umeipata maana kuna wengine hata kupitia wadhamini hawapati tena ikiibiwa.

Kama una uwezo irekebishe then uza. Usimtaabishe Bi. Mkubwa wa watu kwa kumpa tabu kwa jambo ambalo pengine wala hakuusika nalo.
Amina
 
Kwenye ule uzi mwingine nilikupa wazo la kumkamata mdhamini wake, Ila inaonekana una huruma sana ilibidi alivyopiga simu umwambie ailete bajaji kituoni la sivyo mama yake atazidi kukaa ndani. Ila inaonyesha una huruma sana hatuwezi kukupangia cha kufanya
 
Guys, hivi juzi nilikuja na uzi wa kuibiwa bajaj yangu, leo bajaj nmeipata baada ya kumpeleka mdhamini mahakamani na mwizi wa bajaj akaamua kuitelekeza mahala na kupiga simu akatoa location sehemu alipoiacha bajaj, nimefatilia sehemu hiyo mpaka kufika, nimekuta bajaj imeshachakaa sana, imeshakua mbovu na haiwaki.

Inshort ni kuwa inahitaji service ya hali ya juu sana mpaka iweze kurudi kwenye uhafadhari.

Naombeni ushauri wenu, niendelee kudeal na mdhamini wake ambae ni mama yake ili aweze kugharamia service ya hii bajaj.? Ama nifanye nini?

=========
Soma Pia: Naipataje Bajaj yangu iliyoibiwa

KAMA BAJAJI ULIIOKOTA AU ULIPEWA BURE BASI WASAMEHE.LAKINI Km ulinunua deal na MDHAMINI,MGAWANE HASARA.WEWE NUSU YEYE NUSU
 
Back
Top Bottom