BAJAJI KUPAKI KATIKATI YA BARABARA

masatujr1985

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,984
2,000
Kumeibuka tabia sasa waendesha BAJAJI wana-park bajaji zao barabarani hasa sehemu zenye vituo vya mwendokasi (mfano hapa Kimara Korogwe).

Matokeo yake bajaji zinasababisha gari zitumie njia moja na hivyo kusababisha foleni ambayo haina msingi na alhali taffic officers wakiwa kando ya barabara wakiongoza magari!!!

Hii ni kero kwa watumiaji wa hii barabara. Mamlaka zinazohusika ziliangalie hili suala na kulitatua kuondoa usumbufu na hata hatari zinazoweza jitokeza kwa sababu ya matendo ya matumizi mabovu ya barabara.

Natumai kupitia Jukwaa hili wahusika watakuwa wamepata ujumbe na watashughulikia.

Wakatabahu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom