Baharia wa Ukraine akamatwa akitaka kuizamisha boti inayomilikiwa Mrusi Nchini Hispania

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mbaharia mmoja wa Ukraine amekiri kujaribu kuizamisha boti inayomilikiwa na mkuu wa kampuni ya silaha ya serikali ya Urusi, kwa lengo la kulipiza kisasi kwa uvamizi wa Ukraine.

Boti hiyo yenye urefu wa mita 48 sawa na futi 157 inayoitwa Lady Anastasia inamilikiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Rosoboronexport, Alexander Mikheev ilikuwa imetia nanga Majorca nchini Hispania wakati baharia huyo mtaalamu wa ufundi alipofungua ‘valves’ katika chumba chake cha injini.

Alikamatwa na maafisa wa ulinzi Jumamosi Februari 26, 2022 na baadaye kuachiliwa kwa dhamana.

Alimwambia jaji kwamba hajutii chochote na angeweza kufanya hivyo tena.

Mtu huyo alisema alijaribu kuizamisha boti hiyo baada ya kutazama taarifa za habari kutoka Ukraine kwenye televisheni.

"Kulikuwa na video ya shambulio la helikopta katika jengo moja mjini Kyiv. Walikuwa wakishambulia watu wasio na hatiam," alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo.

Si mmiliki huyo, Mikheev au kampuni yake ya Rosoboronexport iliyojitokeza kusema chochote.


Source: bbc

_123447524_gettyimages-1209750344.jpg


=========================================================

Ukrainian sailor in Majorca tried to sink yacht of Russian boss​


A Ukrainian sailor has admitted trying to sink a yacht owned by the head of a Russian state arms firm, in retaliation for the invasion of Ukraine.

The 48m (157ft) Lady Anastasia, which belongs to Rosoboronexport director general Alexander Mikheev, was docked in Majorca in Spain when the mechanic opened valves in its engine room.

He was arrested by Civil Guard officers on Saturday and later released on bail.

He told a judge that he regretted nothing and would do it again.

The man said he tried to scuttle Mr Mikheev's yacht after watching news reports from Ukraine on the television,

"There was a video of a helicopter attack on a building in Kyiv," he was quoted as saying by local media.

"They were attacking innocents."

On Saturday, a high-rise apartment building near Kyiv's Zhuliany airport was hit by a missile, leaving a hole covering at least five floors.

There was no immediate comment from Mr Mikheev or Rosoboronexport, which exports Russian defence products, including tanks, fighting vehicles, aircraft, ships, weapons and ammunition.
 
Back
Top Bottom