*BADO TUNAKUKUMBUKA EDWARD MORINGE SOKOINE*
April 12 unatimiza miaka 34 tangu ulipotutoka ghafla Mpendwa wetu Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine katika ajali mbaya ya gari iliyotokea mkoani Morogoro wakati ukitokea Bungeni mkoani Dodoma.
Daima hautasahaulika na wahujumu uchumi ambao ulipambana nao vilivyo wakati walipotaka kulichezea Taifa kwa kuficha bidhaa muhimu na adimu ili waje wazilangue kwa kuuza kwa bei kubwa. Haukukubaliana na hali hiyo, ulianzisha Mara moja mapambano ya nyumba kwa nyumba kwenda kuwafichua na kukamata bidhaa walizozificha. Hawatakaa wakusahau.
Daima utakumbukwa na majangili na wavamizi wa misitu ambao nao uliamua kuwashughulikia vilivyo kutokana na kuchukizwa na ukorofi wao wa kuunguza miti na misitu. Ulichukizwa sana kutokana na utajiri wa Watanzania kuchezewa vilivyo, ulihakikisha sheria inawabana wanaohusika kuharibu mazingira.
Utakumbukwa na Wabunge kwa namna ulivyowakatalia kata kata kuwaongezea posho na marupurupu ya vikao bali ulikubali kuwaongeza pesa ya chakula tu.
Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano aliyekataa kujilimbikizia Mali bali alikubali kupunguza Mali zake ili aweze kuwatumikia vyema Watanzania.
Utaendelea kukumbukwa daima na Watanzania kutokana na uzalendo, ushujaa na nia ya dhati ya ujenzi wa Taifa la Tanzania. Ni viongozi wachache sana nchini wenye roho na kariba kama yako.
Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano ambaye daima alisimama upande wa umma.
Hakika, Edward Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa kwani aliishi kama ambavyo alikuwa akiyahubiri.
*Shilatu E.J*
View attachment 735942