chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 13,991
- 24,145
Uwaziri Mkuu wa Sokoine ulikuwa wa hovyo kuliko mawaziri wakuu wote tangu nchi ipate uhuru mpaka sasa.
Ni yeye, kama alivyosema Mzee Warioba, aliasisi sheria za hovyo kabisa, hovyo kabisa ambazo zilikiuka haki za binadamu. Utesaji mkubwa ulifanyika na yeye akiwa anangalia.
Upande wa uchumi, mali za watu ziliporwa, watu wakafilisiwa, biashara zilikufa nchi nzima. Hakika yeye ndiye kiini cha uharibifubwa uchumi wa nchi, badala ya kuujenga. Imagine nchi inatoka vitani, halafu ikawa chini ya Sokoine. Yeye akiona duka, anamkamata mwenye duka na kutaifisha bidhaa. Watu wakamwaga sukari katika mito na bahari, watu wakatupa hela maporini. Ulikuwa uongozi wa hovyo kabisa kuwahi kushuhudiwa, mbali na ule wa JPM.
Sioni chochote cha kujivunia kutoka kwake. Urathi wake umeandikwa na Salva Rweyemamu, sikutarajia afanye critical analysis ya uongozi wake zaidi ya kupuliza maumivu waoiyopitia watanzania.
Hii project ya uongozi Institute ni kama iko structured na iko scripted. Tunasubiri urathi ambao utamjadili Sokoine kwa uhalisia wake.