Useful thread!
Kwenye post yako nimeipenda hii......."viongozi wetu wanachelea anasa za mashangingi waliyolazimisha kujinunulia kwa jasho la wananchi masikini. wanajiita waheshimiwa, wanajitutumua kuchoma nyavu za kuvulia samaki ili waonekane "wachapa kazi", lakini mwisho wa siku hawana cha kujishaua mbele ya watanzania kuwa wamelitumikia taifa lao......" Je hawa wanatoka chama gani wanaoogoza kwa hayo? kiongozi wao ndio waliosababisha tukichukie chama kwa kushindwa kuchukua hatua kwa watu kama hawa na akiwemo yeye mwenyewe.
Kuchoma makanisa na kidumu Chama cha Mapinduzi kuna uhusiano gani? We unafikiri ni CUF ndiyo wanaochochea hayo?
wapendwa,
nimehuzunishwa na habari za kuchomwa moto makanisa huko Zanzibar!
napenda kusema kuwa, kanisa laweza kuchomwa moto na hata biblia pia!
kisichoweza kuchomwa moto ni Mungu tu. wale maaskari wa kiyahudi walipijitahidi kumuua Mwana wa Mungu kwa ruhusa ya pilato aliyeshinikizwa na wakuu wa mafarisayo, lakini waliishia kukiri kuwa "alikuwa Mwana wa Mungu"
sasa niwatoe hofu kabisa wapendwa, acheni makanisa yachomwe moto. nyie kesheni katika sala mkijua kuwa shetani katoka kifungoni na anajiua kuwa ana muda mchache tu!!
zaidi sana nawakazia mzitazame siasa! wanasiasa wetu wamekosa weledi wa kufanya siasa na sasa nawafanya "mambo ya siasa"!! muungano wetu umeachwa bila maelezo ya kuwa una faida gani? vijana wasio na kazi, pesa wala akili, wanadanganywa kuwa wakivunja muungano watapata pesa toka OIC na jumuiya nyingine za kiislamu; na zitawawezesha kuwa matajiri!
viongozi wetu wanachekelea anasa za mashangingi waliyolazimisha kujinunulia kwa jasho la wananchi masikini. wanajiita waheshimiwa, wanajitutumua kuchoma nyavu za kuvulia samaki ili waonekane "wachapa kazi", lakini mwisho wa siku hawana cha kujishaua mbele ya watanzania kuwa wamelitumikia taifa lao.
siasa yetu imekufa, imebaki "biashara ya siasa"!
hebu tuamke, tuamke kuipigania nchi yetu!
Mungu ibariki Tanzania, ibariki Afrika,
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
bado nakiamini Chama Cha Mapinduzi, kinaweza kutukomboa!
Glory to God!
Umeongea mambo mengi mazuri,lakini sijaona sababu yeyote ya msingi kwanini unakipenda chama cha magamba,chama kinachokaribia kuzikwa.Amka bwana,CCM hakina jipya kwa watanzania.
Una Imani na Chama Mfu?
Ms. Judith,
umekiri mwenyewe kuwa viongozi wetu wanatumia mashangingi kwa anasa, na hapo hapo umesema bado unaiamini ccm.
Unatuchanganya mummy! Funguka bana
Content katika thread yako ni nzuri, ningefurahi zaidi kama ungebadilisha heading! Hapo naona umeharibu.... ahh labda nawe kwakuwa una haki pia. Na ulivyomalizia pia uliharibu zaidi, Hayo maneno "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI" yananikumbusha wakati niko darasa la pili, hata akifika katibu wa kata shuleni mnaimba hizo nyimbo, lakini siku za leo nikisikia huwa napata machungu sana. Maana ninapopita mtaani na kuona watu wanalalamika na maisha nathubutu kusema ni CCM. Nikiona mtu anakosa mlo mmoja kila siku pia nazidi kupata uchungu zaidi.wapendwa,
nimehuzunishwa na habari za kuchomwa moto makanisa huko Zanzibar!
napenda kusema kuwa, kanisa laweza kuchomwa moto na hata biblia pia!
kisichoweza kuchomwa moto ni Mungu tu. wale maaskari wa kiyahudi walipijitahidi kumuua Mwana wa Mungu kwa ruhusa ya pilato aliyeshinikizwa na wakuu wa mafarisayo, lakini waliishia kukiri kuwa "alikuwa Mwana wa Mungu"
sasa niwatoe hofu kabisa wapendwa, acheni makanisa yachomwe moto. nyie kesheni katika sala mkijua kuwa shetani katoka kifungoni na anajiua kuwa ana muda mchache tu!!
zaidi sana nawakazia mzitazame siasa! wanasiasa wetu wamekosa weledi wa kufanya siasa na sasa nawafanya "mambo ya siasa"!! muungano wetu umeachwa bila maelezo ya kuwa una faida gani? vijana wasio na kazi, pesa wala akili, wanadanganywa kuwa wakivunja muungano watapata pesa toka OIC na jumuiya nyingine za kiislamu; na zitawawezesha kuwa matajiri!
viongozi wetu wanachekelea anasa za mashangingi waliyolazimisha kujinunulia kwa jasho la wananchi masikini. wanajiita waheshimiwa, wanajitutumua kuchoma nyavu za kuvulia samaki ili waonekane "wachapa kazi", lakini mwisho wa siku hawana cha kujishaua mbele ya watanzania kuwa wamelitumikia taifa lao.
siasa yetu imekufa, imebaki "biashara ya siasa"!
hebu tuamke, tuamke kuipigania nchi yetu!
Mungu ibariki Tanzania, ibariki Afrika,
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
bado nakiamini Chama Cha Mapinduzi, kinaweza kutukomboa!
Glory to God!
mpendwa,
kwa kujibu swali lako, nasema "yes",
nina imani na Chama cha Mpapinduzi!!
CCM si chama mfu, CCM kitashiunda tena uchaguzi wa 2015, kitashika dola tena!! na kwa mshangao wako, hao "wafu" unaowaona CCM hawatakuwepo tena, watakuwa wameishaondoka na makundi ya "wafu" wenzao. sisi tulio hai tutakaokuwa tumesalia tutakuwa pamoja na watanzania wenzetu nchi nzima tukiujenga uchumi wa kijamaa kwa manufaa ya jamhuri ya muungano wa tanzania na watu wake wote!
kidumu Chama Cha Mapinduzi!!
mbarikiwe sana wapendwa,
Glory to God!