Leo ni mara yangu ya kwanza kuleta mada hapa na ninakiri kuwa nilikuwa msomaji tu wa kawaida.
Nina tatizo kubwa linalonisumbua kwa sasa. Mimi ni mwanamke. Nilikuwa na mpenzi tuliedumu nae mwaka mmoja na nusu, mimi nikimpenda kweli ila sijui kwa mwenzangu ingawa naye nilizoea kusikia akiniambia hivyo. Miezi miwili iliyopita tuligombana.
Chanzo ikiwa ni yeye. Akidai kuwa anahitaji kuwa huru tu ingawa hana msichana mwingine. Niliomba msamaha kwa yote niliyomfnyia mpaka kufikia huko lakini hakuridhia. Tukaachana ila tukiendelea kuwasiliana na kusaidiana kama zamani. Ukaribu bado ulikuwepo ila haukua ule wa kimapenzi.
Mwenzangu aliendelea kuwa na furaha na hata mara nyingine aliongea vitu ambavyo nilihisi alitaka nimwonee wivu. Hali hiyo ikanikera na tukagombana tena na kumtukana juu. Ukaribu wetu ukapungua kwa kiwango kikubwa na hata simu hatukupigiana kwa muda wa mwezi mmoja.
Kiukweli nilimmisi muda huo nikatamani tena niwe karibu nae. Jana usiku nimempigia simu na kumuomba samahani, cha ajabu ananiambia yeye hana shida kabisa na mimi na bado anapenda kuwa karibu yangu. Usiku mzima ananitumia message kunitania hili na lile ingawa si za kimapenzi.
Hivi huyu mtu bado ananipenda kweli?
huyo anataka tu kuwa na wewe.. mgegedane but hana mpango wa kukuoa.. katumia ustaarabu wa kujiweka pembeni ili kukupa chance ya kumpata mwingne mwenye nia ya kukuoa.. maana anakuhurumia kukwambia hanampango wa kukuoa.. wanaume wengi wazuri sana wa kumpotezea muda mdada mwenye nia ya ndoa.. anakua nae anamuigizia mapen ya kweli kumbe hana hizo mambo za kuoa ye ni papuch tu.
so tafakar unahitaj nin kwake..
Jamaa ana roho nzuri sana anajaribu kukuambia kwa vitendo wewe unashindwa kujiongeza.Kiukweli hapendi uwe mpenzi wake ndio maana amekuachia nafasi ila wewe unapenda watu kiboya, tafuta mpenzi.....huyo jamaa mtaeendelea kusaidiana kama marafiki
Umewekwa pending tu ili yakimshinda huko alikoenda apate pa kupoozea maumivu, come on mimi naamini thamani yako ni kubwa zaidi ya hiyo, usikubali mtu akufanye kama toy la kuchezea, mwambie a-hang hapo kisha songa mbele