Bado anamkumbuka marehemu mkewe

kidaganda

JF-Expert Member
Aug 26, 2013
2,995
2,571
Habari wana MMU
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,Nina rafiki yangu ambaye ameolewa na Mwanaume ambaye alifiwa na mkewe miaka kadhaa iliyopita.

Anasema mwanzoni alidhani mumewe huyo bado yupo kwenye majonzi ya kumpoteza mkewe aliyefariki. Ila kadri siku zinavyozidi kwenda jamaa ameendeleza tabia zake hizo ambazo amezita.

i)kujifunika shuka alizonunua na marehemu
ii)kukumbatia na kubusu picha za marehemu

Anadai zipo tabia kadhaa ila hizo zimekuwa zinamfanya ajione asiye na thamani Kwa huyo mmewe..

Yeye ameamua aondoke aachane nae nyie mnashauri vipi.

Karibuni tumshauri dada yetu.
 
Ukiolewa kwa lengo la kuziba kiraka unakua kiraka tu na lazima ujue wewe ni kiraka tu ukishajijua unakua huna stress. Sasa yeye anataka aishi kama mke wa zamani?

Chagua moja kua kiraka au uwe mpya kwa mume mwingine
 
Avumikie tu!!! Kupoteza mpenzi sio jambo la kusahaulika kirahisi... Wakati anaolewa si alijua hiyo historia? Basi aendelee tu kumfariji
 
Kafiwa Jackie Kennedy na kaendelea na maisha yake mpaka kaolewa tena na Aristotle Onassis.

Huyo mwanamke.

Mambo mengine ni kujiendekeza tu.
 
Ndo maana amemuoa ili amfariji na sio kumshangaa. Ajitahidi kumsahaulisha machungu ya kuondokewa na mke na sio kusubiri mfiwa aanze kumbembeleza yeye.
 
Kuondoka kwake inamaanisha ajakomaa kiakili,..ii anayofany mumewe sio tabia,ni mazoea,..kwa iyo anchotakiwa kua na subira au kumpa mapenzi uyo mume mpaka apagaw asahau mkewe,..mbona mkiwa mchepuko hamjiulizi aya maswali!?
 
Habari wana MMU
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,Nina rafiki yangu ambaye ameolewa na Mwanaume ambaye alifiwa na mkewe miaka kadhaa iliyopita.

Anasema mwanzoni alidhani mumewe huyo bado yupo kwenye majonzi ya kumpoteza mkewe aliyefariki. Ila kadri siku zinavyozidi kwenda jamaa ameendeleza tabia zake hizo ambazo amezita.

i)kujifunika shuka alizonunua na marehemu
ii)kukumbatia na kubusu picha za marehemu

Anadai zipo tabia kadhaa ila hizo zimekuwa zinamfanya ajione asiye na thamani Kwa huyo mmewe..

Yeye ameamua aondoke aachane nae nyie mnashauri vipi.

Karibuni tumshauri dada yetu.
 
Huyo mwanamke anatakiwa kuwa faraja, kufanya kila awezalo kupunguza machungu,
Napia asiwe na wivu na marehemu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom