Badilika kulingana na mabadiliko

Badilika kulingana na mabadiliko

boniuso

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
924
Reaction score
1,291
Kwa wastani binadamu huwa mwenye fikra 12000-50000 kwa siku ambapo katika fikra hizo 80% ya mawazo hayo na fikra hizo ni hasi huku asilimia zingine ndio chanya.

Kwa wastani wa 80% ya fikra hasi kwa siku ndio sababu 80% ya watu duniani hawana furaha huku wakisumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo.

Wengi wanateseka kwa msongo wa mawazo bila wao kujua sababu za chanzo.

Kwa kufuata wastani huo ni kuwa ukipata tatizo lolote zaidi ya 80% ya watu utakaowaambia tatizo lako hawatakusaidia.

Binadamu huwa hajifunzi chochote pale anapoamini kuwa anajua anachofundishwa.

Dunia yetu imegawanyika kwa aina mbili za watu ambapo wapo extrovert ambao ni 75% na Introverts ambao ni 25%.

Extrovert ni watu wanaongea kwanza kisha wanafikiri baadaye,huwa wenye marafiki wengi sana,huwa wanapenda kujumuika pamoja katika sherehe.

Hupenda mazungumzo ya hapa na pale ambapo unaweza kukaa nao masaa mawili au zaidi huku hamna habari maalum.

Hupata marafiki haraka na kuwapoteza haraka,hutoa ahadi haraka na kuvunja baada ya kutafakari.

Introverts huwa wapole, huongea kidogo na kufikiri sana, hawana marafiki wengi, hudumu kwenye mahusiano,huwa hawatoi ahadi .haraka,ukiwashtkiza swali huwa hawana cha kujibu, husahau sana vitu vidogo.

Ukishatambua kuwa upo kundi gani ni hatua nzuri sana ya kuwa na furaha.

Watu wengi huwa wanahusisha mafanikio ya kiuchumi, umaarufu, marafiki wengi, muonekano wa maumbile, mahali za kuzaliwa, rangi, cheo, ukoo, kiwango cha elimu kama kipimo cha thamani yao.

Ukweli ni kuwa thamani yako haipo kwenye cheo, umaarufu, rangi, lafudhi, mahali pa kuzaliwa, muonekano wa sura au umbo,wingi wa fedha au mali, kuwa na mwanaume au mwanake mzuri.

Badala yake furaha yako ipo kwenye fikra zako tu.

Hii ndio sababu watu ambao wapo kwenye nchi unazotarajia wangekuwa na furaha wala hawana furaha.

Watu ambao unatarajia waishi kwa furaha kila siku hawana furaha.

Kitendo cha kukosa furaha kila siku hupelekea magonjwa yasiyoambukiza kama madonda tumbo, kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu.

Pamoja na matatizo kama kukosa hamu ya kula, uchovu, uzee, kukosa usingizi, kuvurugika kwa hedhi, kupata polycystic ovary syndrome, kinga ya mwili kushuka, baadhi ya kansa,kuchochea asthma, magonjwa ya ngozi kwa sababu ya kinga kushuka

Badala ya kuwalaumu watu kwa tabia zao waelewe watu vile walivyo sio vile unavyowaona.

Watu wengi wanajua kuhukumu sana kuliko kufikiria.

Wengi wakiona kitu hawakuelewi hawaulizi bali hujenga kichwani majibu yao wenyewe na kuwaaminisha wengine.

Watu wengi wana hasira hivyo ukowakosea kidogo watadhihirisha hasira yao.

Kama ulikuwa hujui kile mtu huongeaa anaongea kama kiwakilishi cha fikra zake sio uwepo wako.

Mtu mwenye kauli nzuri ukimkosea atakujibu kwa kauli nzuri na ikiwa umemkosea mtu mwenye hasira atakujibu kwa hasira.

Mtu akikuahidi kisha akatekeleza anafanya hivyo kwa sababu ya tabia yake sio kwa sababu wewe ni special.

Mtu atakulaumu kwa kile umefanya au hukufanya kwa sababu ya tabia yake sio kosa lako.

Mtu mwenye upendo wa dhati atakuonyesha upendo wa dhati hata pale unapokosea na mwenye chuki atakuonyesha chuki hata kama utafanya wema.

Maoni ya watu ni tafsiri ya kile kipo kwenye akili zao sio kile umefanya au hukufanya.

Watu hutoa maoni tofauti kwa jambo moja sio kwa sababu jambo limebadilika bali fikra za watu hazifanani

Watu wengi hawana maarifa sahihi juu ya nini wafanye nyakati ngumu hivyo wengi hudhihirisha hasira zao

Wapo watu hata ukiwapa vitu vyote ulivyonavyo kisha wewe ukakosa bado watakulaumu

Mtu kutosheka au kuacha kutosheka ni maamuzi yake wala sio kile umefanya

Mtu kushukuru au kuacha kushukuru ni tabia yake sio kile umefanya

Mtu kusamehe makosa ya wengine ni tabia yake wala sio makosa watu wamefanya

Wapo watu hata akisikia mtu anatafuna hupata hasira tatizo sio kutafuna bali hasira walizonazo muda mrefu

Wapo watu unaweza kuwakosea leo kisha kosa hilo watakulaumu kila siku hata kama umeomba msamaha na kusamehewa

Mtu asiejipenda hata akipendwa na dunia nzima bado anahisi hakuna anaempenda.

Elewa watu vile walivyo sio vile unaowana

Watu watakulaumu endapo utafanya maamuzi tofauti na matarajio yao

Kila unapoweka matarajio kwa watu unakuwa unataka kuvunjwa moyo

Watu watakuvunja moyo kwa sababu ya matarajio yako mwenyewe unayoweka juu yao

Kama utaondoa matarajio kwa watu utakuwa umeondoa nguvu yao ya kuziumiza hisia zako

"No expectations no disappointment"

Huzuni ni tofauti ya matarajio na uhalisia kama matarajio ni makubwa huzuni inakuwa kubwa

Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)

6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)

+255766862579
+255622414991

Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam
 
Kwa wastani binadamu huwa mwenye fikra 12000-50000 kwa siku ambapo katika fikra hizo 80% ya mawazo hayo na fikra hizo ni hasi huku asilimia zingine ndio chanya...
Ahsante mkuu kwa elimu hiyo ya kweli,nitakutafuta.
 
Hakika mtu aliyeishi haya furaha I ndani mwake hata kama atalala na njaa
 
Back
Top Bottom