Habari za kazi wanajamvi.
Samahani, miongoni mwa kozi nne alizopata bwana mdogo katika maombi ya vyuo vikuu kwa msimu wa masomo wa 2022/2023 ni pamoja na kozi tajwa hapo juu (Bachelor of Security and Strategic Studies at Institute of Accountancy Arusha (IAA)
Binafsi nimetamani kuijua kozi hii kwa undani kwa sababu dogo ni kama amekuwa interested nayo sana.
Tafadhali kama kuna yeyote anaifahamu vizuri naomba japo maelezo na maelekezo kidogo na expectations zake baada ya kuhitimu kwa namna ya kujiajiri na kuajiriwa, ushindani katika soko ukoje na mengineyo ya ziada.(kama yapo)
Natanguliza shukrani zangu za dhati sana.