Babu ni mganga wa kienyeji kama waganga wengine tu. Inanisikitisha sana kuona bado kuna watu wanashabikia udanganyifu huu mkubwa. Kisayansi, dawa haijathibitishwa na watu wanaendelea kufa. Kiimani anadai eti kaoteshwa na Mungu, uongo mkubwa. Mungu hawezi akafanya jambo kinyume na Biblia. Katika agano jipya Mungu haponyi kwa kutumia miti. Anatumia Neno lake tu. Na Mungu haweki neno kwenye miti, anaweka neno mioyoni mwa watu (Soma Rumi 10:17), hii ndio imani.
Inasikitisha watanzania tumekuwa wepesi mno wa kudanganyika kirahisi namna hiyo bila kufanya utafiti wowote wa kisayansi au kiimani