Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
UKO WAPI BABA YANGU ASKOFU ZACHARY KAKOBE
Injili uliyoihubiri pasipo kuangalia uso wa mtu imehadimika Tanzania!
Kila mkristo (na asiye mkristo) mwenye mapenzi mema na kanisa na taifa la Tanzania, anakufahamu vizuri na kukupenda pia!
Nakukumbuka kwenye miaka ya 90 ulipokuwa ukihubiri Injili ya toba na hata kwenye miaka ya 2000 ulipokuwa ukifundisha neno la Mungu lisiloghoshiwa kabisa. Wahubiri uchwara walikugwaya sana na kukuinulia vikwazo na tuhuma za hovyo, lakini wengi wao walikuja kwako pale Mwenge kutubu miaka michache baadaye.
Nakumbuka maneno yako uliyowaambia wachungaji na maaskofu wa kipentekoste, pale Askofu Dr. Arthur Gitonga wa Kenya, alipowataka maaskofu na wachungaji waliokushambulia kwa maneno makali pale ulipoihubiri FULL GOSIPLE pasipo kupamba dhambi makanisani, watubu; Ulisema, "Hapana. Sioni sababu ya wao kuniomba msamaha.
Wanajijua, lakini Bwana aliona vema niudhiwe na ndugu zangu kama Yusufu!" hata hivyo walitubu kwa machozi na uliwasamehe kabisa!
Baba Askofu, Wewe ulipajua vyema alipokutoa Bwana. Kwenye uchafu wa kila aina. Kwenye kukata mauno ambayo wewe uliita 'Ngwasuma' na maisha ya ajabu ajabu. Hukutaka kurudi kule ulikotolewa. Uliipenda madhabahu na kamwe hukutaka kuinajisi kwa kuhubiri vitu vya ajabu ajabu ukiviita neno la Mungu. Ulimuheshimu Mungu naye akakuheshimu!
Nani akane kuhusu mkono wa Bwana uliokuwa juu yako uliokuwezesha kuhubiri Injili iliyo hai iliyowapeleka maelfu kwa maelfu ya wenye dhambi kwa Yesu ndani na nje ya bara la Africa!
Nani akane ishara za Roho Mtakatifu zilizokufuata kila ulipoenda?
Baba, njoo tena Tanzania. Wale uliowakemea miaka ile washarudi kule kule ulikowatoa. Hakuna wa kuwakemea. Wachungaji, Mitume na manabii wachache sana wanaihubiri kweli siku hizi, wengi ni wachuuzi. Wanaitumia Injili kuibia mamia ya wenye shida. Wanajifanya miungu watu. Wapo wanaofundisha kusema ili usamehewe lazima utoe sadaka ya dhambi!
Wengine wanasema ili upokee muujiza sharti ulale nao. Baba, yapo mengi. Ukishuhudia yanayotendeka madhabahuni baba utalia. Wale waliobaki na kweli hawakemei wapotofu. Wanaojitahidi kukemea wanasongwa na manyang'au eti 'wasihukumu!'
Waimbaji wanaojiita watumishi waimba muziki wa Injili sasa hivi wamewaleta kina Ngwasuma uliowakataa kabisa. Sasa wanakata viuno madhabahuni na huwezi amini macho yako kama haya yanatendeka kwenye kanisa la Tanzania, tena mbele za wachungaji wenye majina makubwa na heshima mbele za jamii.
Baba, hata Serikali sasa hivi haigopi mtu wala kitu. Hakuna anayekemea upotofu na uovu wa serikali na wanasiasa. Wamemuachia mchungaji Gwajima peke yake naye nahisi huenda akanyamaza au naye akaamia zake Japan 'kwao' kwa kuwa hana wa kumsaidia kukemea!
Baba, utakuja lini Tanzania? Nakusubiri kwa hamu na ukitua uwanja wa ndege wa KIA au JKNIA nitakuwa wa kwanza kukupokea na kukuomba utoe kauli na msimamo wako kuhusu hali hii maana wanao tunaumia tunapoona madhabahu ya Bwana ikinajisiwa. Hatuwezi kwenda mbali pasipo utakatifu. Pesa na mali tukipata vitatufaidia nini ikiwa tutaikosa Mbingu sisi na tunaowachunga?
Bado nipo magotini!
Na uje Bwana Yesu!!!!