Baba mwenye nyumba ajinyonga hadi kufa baada ya kuchukuliwa ndama na vikoba

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Kina mama na kina dada mlio olewa acheni kuchukua mikopo bila ya kuwashirikisha waume zenu, mnafanya siri mwisho wa siku siri inasanuka.

Imetokea mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Hai, kuna Mama ambaye alikuwa mwanachama wa kikoba (jina kapuni) alienda kuchukua mikopo dhamana ikiwa ni ndama ambao alipiga picha muda ambao mzee hakuwepo na hivyo kusema ndama hao ndio dhamana kwenye mkopo. Ilipofika siku ya marejesho mama alishindwa kurejesha mkopo ilibidi wana kikundi wa kikoba waje wachukue ndama hao waenda kuwauza ili wapate pesa zao za mkopo, muda huo huo mzee alikuwa ndio amefika kutoka kukata majani ya hao ndama ili awalishe alivyoingia tu akakutana na wanachama hao wa vikoba wakitoka na ndama hao wakidai mama ameshindwa kulipa mkopo, mzee alimuuliza mkewe kama ndio maisha hayo waliyokubaliana nae hakuwa na jibu mwisho mzee aliingia ndani na kuchukua kamba akajinyonga akafa maana alikuwa ameshachoka na maisha na huenda kuna tabia zilikuwa zimemchosha kwa siku nyingi. mzee atazikwa leo au kesho.

Je kwenye huu msiba huyu mama atalia au hatalia kwa kumpoteza mumewe.
 
Mzee alikuwa ameshachoka na maisha asisingizie ndama
 
Kuhimii mshtuko kunahitaji moyo hasa, vinginevyo ndio hayo. Kuna mtu anaingia chumbani anakuta wife anashonwa na baba mwenye nyumba, anaenda bar kunywa akirudi nae anashona, siku zinasonga. Mzee kabebewa ndama, kajinyonga.
 
Back
Top Bottom