MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,460
- 69,385
Ukimsikiliza Raisi Mugabe alikuwa na akili sana na anajua nini anachofanya,
Lakini baada ya kuwa Rais kuna kitu hakikwenda saana na yeye akabadilika na kuwachukia sana Wazungu tofauti na alivyotabiliwa mwanzo.
Mzee Nyerere alitofautiana sana na wazungu lakini aliweza kuitawala chuki yake ambayo iliwameza sana viongozi wengi wa Afrika hasahasa wale wa Mlengo wa kijamaa. Tukubali hawa jamaa walitutawala lakini ikumbukwe pia kwamba wazungu wema pia wapo.
Yote tisa,
Mzee Wetu Mugabe alikosea akawaumiza watu wake, huu ndiyo udhaifu wake wa kibinadamu.
Lakini ninachokiamini ni kwamba Mchango wake na Upendo wake kwa Bara la Afrika ni mkubwa sana na Upendo wake kwa Africa siyo wa kutiliwa shaka.
NB 1: Nimefurahi kuona Zimbabwe ina Rais mpya lakini kilichonivunja moyo ni mbinu waliyoitumia kumuweka huyo Rais mpya. Kisiasa Zimbabwe bado ni nchi changa kiutawala na imetawaliwa na Rais moja tu toka Ian Smith hivyo kuwafundisha watu kwamba mtutu wa bunduki ndiyo suluhu inaweza kuwajengea saikolojia mbaya sana watu wa Zimbabwe.
Upande wa Pili Demokrasia ya Kwenye Vitabu na Demokrasia katika maisha ya kila siku ni vitu viwili tofauti sana. Zimbabwe haitajiita nchi ya Kidemokrasia kwasababu tu Mugabe ametoka kwenye nafasi ya Urais na wamepiga kura kuchagua viongozi wapya.
Kujenga Demokrasia kunatumia muda mrefu sana na siyo mwaka kama ambavyo wengi wetu wanajiaminisha. Sifa moja kwenye Demokrasia yoyote iliyokomaa ni:
Lakini ukiangalia historia ya nchi ile utaona Demokrasia waliyonayo sasa hivi ni tofauti kabisa na ile ya Kipindi cha Abrahama Lincoln au Andrew Jackson (Imekuwa na wao walijenga mazingira hayo)
Demokrasia ni lazima nayo iwe na mipaka na iendane na hali halisi ya kiutamaduni ya nchi husika. Leo hii ukisema kwamba Rais achaguliwe kwa kupigiwa kura tu watu wengi tunaweza kujenga taifa baya sana na kuhatarisha hata Usalama wa nchi. Ndiyo maana mababa wa taifa la Marekani wakiongozwa na Rais Thomas Jefferson waliona hii hatari ya TYRANNY OF NUMBERS hasa kwenye nafasi kama ya Urasi: Wakaona kwamba siku anaweza akaingia mwanasiasa ambaye anajua kucheza na akili za watu (A demagogue, A sophist and An Opportunist) na akateuliwa na mwisho wake akaja kuharibu nchi. Kuzuia hili waketengeneza THE ELECTORAL COLLAGE.
NB 2: Upande wa pili wa shilingi ni kwamba,
Wamarekani wanahubiri demokrasia kwa mataifa mengine lakini nao wamechukua muda kufika hapa. Katiba yao inaanza na Kusema "WE THE PEOPLE" lakini katika uhalisia wa mambo "WE THE PEOPLE" ilikuwa inamaanisha makundi haya yafuatayo:
Tena Wanawake waliruhusiwa kuanza kupiga kura baada ya mwaka 1918, na mwisho kabisa Weusi wameanza kuonwa kama ni Binadamu nchini Marekani mnamo miaka ya 1960's.
Hivyo Demokrasia huwa haiji kama Mana au Kware kutoka mbinguni.,
Inabidi injengwe kwa kuachiwa mazingira ya kukua; Wananchi tuaminiane na tuache ubinafsi.
NB 3: Afrika tatizo siyo watawala tu,
Hata raia tumechangia sana kwa kukwamisha maendeleo ya demokrasia.
Mchekeshaji George Carlin alishawahi kusema "I don't hate politicians, because they are the product of a society they live in" Hivyo ninadiriki kusema leo kwamba tabia ambazo viongozi wa nchi wanazo ndizo ambazo raia wake wanazo kwa wingi. Tabia nyingi za mtu huwa hajifunzi ukubwani, huwa zinajengwa tangu utoto wake.
Hivyo ukiona Raisi ni mtu mwenye tamaa ni lazima ujue ile ni tabia ambayo iko kwenye jamii yake kwa kiasi kikubwa. Sababu kubwa ni kwamba kama jamii inajielewa basi tabia ya wizi ni lazima ingekemewa kuanzia kwenye ngazi za familia hadi kupelekea kuunda jamii yenye watu ambao wanachukia Rushwa kwa kiasi kikubwa. Tatizo letu hapa Afrika tukiona wizi au udhalilishaji wa kijinsia unafanywa tunaona ni kawaida na wengine hadi hudiriki kusema Makabaila fulani yanaongoza kwa wizi na Makabila fulani yanaongoza kwa kudhalilisha wanawake.
NB 3: Ufisadi Tanzania ni tabia ya wananchi walio wengi.
Na huwa tunakosea sana kudhania Ufisadi au Rushwa ni kwenye mambo ya pesa tu.
Ukienda kuanzia shule za msingi walimu ni mafisadi na wanongoza kuibia sana wazazi na wanafunzi hasa huko vijijini kwa kupitia twisheni au kazi mbali mbali. Mwalimu ambaye amezoea pesa za bure siku atapanda cheo na kuwa Afisa Elimu, Mkurugenzi na hata Raisi. Usitegemee tabia yake ya Rushwa na Ufisadi ataicha hata akiwa Rais. (Itakuwa inashamiri na kukoma kutokana na nafasi anayopata ili aibe vizuri)
Waafrika wengi ni watu ambao sera za Ujamaa zimetuharibu au niseme tumezielewa vibaya,
Wengi wetu hatupendi kufanya kazi na kutegemea Serikali ndiyo itufanyie kila kitu (Haiwezekani). Ukienda kwenye Maofisi ya Serikali ndiyo utajionea mwenyewe. Watu wana muda mwingi wa kukaa kazini lakini wana muda mchache sana wa kufanya kazi. Unakuta mtu anafika ofisini tokea asubuhi yeye yuko mtandaoni tu, kutafuta safari apewe Per Diem na kutegeana saanaaa.
Jamii yoyote isiyopena kufanya kazi ni lazima itakuwa masikini.
Na palipo na Umasikini ni lazima mambo mabaya yote utayakuta.
Mwanafalsafa Karl Marx anasema kuna kitu kinaitwa BASE AND SUPERSTRUCTURE.
Kwamba jambo lolote jema au baya ndani ya nchi hujengwa na hali ya Uchumi wa nchi hiyo.
Anadai kwamba jamii masikini ni lazima itakuwa imetawaliwa na haya yafuatayo:
Hata kama yapo basi ni kwa kiasi kidogo sana hivyo wananchi watakapoamua kurekebisha Msingi wao wa KIUCHUMI kwa aidha kufanya kazi au kuondoa unyonyaji basi hayo mambo yote yataisha (SIJUI KAMA NI KWELI)
NB 4: Mwisho kabisa,
Waafrika ni lazima tufike mahali tubadilike tena tusianzie kwenye ngazi za kisiasa kama ambavyo CHADEMA na CCM wanataka kutuaminisha uongo. Kabla ya mataifa kuzaliwa mwanadamu alianza kuwa na familia kwanza: Nadiriki kusema kwamba Familia Imara ndiyo msingi wa Taifa Imara. A Strong Family: The Foundation of A great nation. Mungu ana akili sana kuumba familia kabla ya Falme na mataifa makubwa.
Marekani na mataifa ya Ulaya yalikuwa na nguvu sana kwasababu ni watu wanojali familia kwa kiasi kikubwa sana. Mzazi anavyofanya kazi anakuwa na jambo moja tu kichwani "Maisha ya watoto wangu" Hivyo inapelekea mzazi kuhusika kwa namna moja au nyingine katika maendeleo ya mtoto kwa kiasi kikubwa.
Ukishambulia familia basi umeharibu taifa, naomba niwape ushahidi wa kihistoria katika hili:
Tatizo kuu la Afrika siyo Utawala pekee na ndiyo maana kumetokea mapinduzi mengi sana yenye kumwaga damu hapa barani kwetu lakini matatizo hayaishi tu. Zimbabwe matatizo yake mengi yameletwa na Mugabe lakini hata akiondoka nina uhakika yatabaki tu...Nigeria kumekuwa na historia ya mapinduzi lakini mpaka leo hii bado kuna matatizo mazito sana.
Hivyo inabidi tubadilike na tujaribu kujifanyia tathmini kwa upya kwamba tumekosea wapi,
Leo nilichofanya hapa ni "FINDING SOLUTION FOR POLITICAL QUESTIONS OUT OF POLITICS"
Tusidhanie kwamba Siasa ndiyo kila kitu na itatatua matatizo yetu, hebu tuvuke mipaka na tujaribu kuangalia upande wa pili wa maisha yetu hasa kwenye vitu vidogo vidogo sana. Mzee Nyerere alifanikiwa sana kwasababu siasa yake iligusa vitu vidogo vidogo sana, familia kupitia vijiji zilikuwa na maamuzi makubwa juu ya hatma ya nchi yao. Tuige, tuboresha, mabaya yake aliyofanya tuyatupe, tuach kulaumu na tusonge mbele.
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania.

- Imani baina ya Watawala na Raia wake (Mutual Trust and Good Faith)
- Taarifa kwa wananchi kuhusu nchi yao (Access to Vital Information of a Polity). Ni jambo la hatari sana kuwapa Raia haki za Kidemokrasia bila wao kujua umuhimu wa hizo haki na madhara yake endapo watazitumia vibaya)
- Uwajibikaji kwa pande zote zinazounda nchi (Responsibility to all stake-holder in Polity)
Lakini ukiangalia historia ya nchi ile utaona Demokrasia waliyonayo sasa hivi ni tofauti kabisa na ile ya Kipindi cha Abrahama Lincoln au Andrew Jackson (Imekuwa na wao walijenga mazingira hayo)
Demokrasia ni lazima nayo iwe na mipaka na iendane na hali halisi ya kiutamaduni ya nchi husika. Leo hii ukisema kwamba Rais achaguliwe kwa kupigiwa kura tu watu wengi tunaweza kujenga taifa baya sana na kuhatarisha hata Usalama wa nchi. Ndiyo maana mababa wa taifa la Marekani wakiongozwa na Rais Thomas Jefferson waliona hii hatari ya TYRANNY OF NUMBERS hasa kwenye nafasi kama ya Urasi: Wakaona kwamba siku anaweza akaingia mwanasiasa ambaye anajua kucheza na akili za watu (A demagogue, A sophist and An Opportunist) na akateuliwa na mwisho wake akaja kuharibu nchi. Kuzuia hili waketengeneza THE ELECTORAL COLLAGE.
NB 2: Upande wa pili wa shilingi ni kwamba,
Wamarekani wanahubiri demokrasia kwa mataifa mengine lakini nao wamechukua muda kufika hapa. Katiba yao inaanza na Kusema "WE THE PEOPLE" lakini katika uhalisia wa mambo "WE THE PEOPLE" ilikuwa inamaanisha makundi haya yafuatayo:
- Waprotestanti (Protestants)
- Wanaume (Male)
- Weupe wenye asili ya Ulaya (White Caucasian Male)
Tena Wanawake waliruhusiwa kuanza kupiga kura baada ya mwaka 1918, na mwisho kabisa Weusi wameanza kuonwa kama ni Binadamu nchini Marekani mnamo miaka ya 1960's.
Hivyo Demokrasia huwa haiji kama Mana au Kware kutoka mbinguni.,
Inabidi injengwe kwa kuachiwa mazingira ya kukua; Wananchi tuaminiane na tuache ubinafsi.
NB 3: Afrika tatizo siyo watawala tu,
Hata raia tumechangia sana kwa kukwamisha maendeleo ya demokrasia.
Mchekeshaji George Carlin alishawahi kusema "I don't hate politicians, because they are the product of a society they live in" Hivyo ninadiriki kusema leo kwamba tabia ambazo viongozi wa nchi wanazo ndizo ambazo raia wake wanazo kwa wingi. Tabia nyingi za mtu huwa hajifunzi ukubwani, huwa zinajengwa tangu utoto wake.
Hivyo ukiona Raisi ni mtu mwenye tamaa ni lazima ujue ile ni tabia ambayo iko kwenye jamii yake kwa kiasi kikubwa. Sababu kubwa ni kwamba kama jamii inajielewa basi tabia ya wizi ni lazima ingekemewa kuanzia kwenye ngazi za familia hadi kupelekea kuunda jamii yenye watu ambao wanachukia Rushwa kwa kiasi kikubwa. Tatizo letu hapa Afrika tukiona wizi au udhalilishaji wa kijinsia unafanywa tunaona ni kawaida na wengine hadi hudiriki kusema Makabaila fulani yanaongoza kwa wizi na Makabila fulani yanaongoza kwa kudhalilisha wanawake.
NB 3: Ufisadi Tanzania ni tabia ya wananchi walio wengi.
Na huwa tunakosea sana kudhania Ufisadi au Rushwa ni kwenye mambo ya pesa tu.
Ukienda kuanzia shule za msingi walimu ni mafisadi na wanongoza kuibia sana wazazi na wanafunzi hasa huko vijijini kwa kupitia twisheni au kazi mbali mbali. Mwalimu ambaye amezoea pesa za bure siku atapanda cheo na kuwa Afisa Elimu, Mkurugenzi na hata Raisi. Usitegemee tabia yake ya Rushwa na Ufisadi ataicha hata akiwa Rais. (Itakuwa inashamiri na kukoma kutokana na nafasi anayopata ili aibe vizuri)
Waafrika wengi ni watu ambao sera za Ujamaa zimetuharibu au niseme tumezielewa vibaya,
Wengi wetu hatupendi kufanya kazi na kutegemea Serikali ndiyo itufanyie kila kitu (Haiwezekani). Ukienda kwenye Maofisi ya Serikali ndiyo utajionea mwenyewe. Watu wana muda mwingi wa kukaa kazini lakini wana muda mchache sana wa kufanya kazi. Unakuta mtu anafika ofisini tokea asubuhi yeye yuko mtandaoni tu, kutafuta safari apewe Per Diem na kutegeana saanaaa.
Jamii yoyote isiyopena kufanya kazi ni lazima itakuwa masikini.
Na palipo na Umasikini ni lazima mambo mabaya yote utayakuta.
Mwanafalsafa Karl Marx anasema kuna kitu kinaitwa BASE AND SUPERSTRUCTURE.
Kwamba jambo lolote jema au baya ndani ya nchi hujengwa na hali ya Uchumi wa nchi hiyo.
Anadai kwamba jamii masikini ni lazima itakuwa imetawaliwa na haya yafuatayo:
- Wizi, Ufisadi, Rushwa na unyang'anyi wa kila aina.
- Ukahaba watu kuuza miili yao.
- Chuki.
- Magonjwa
- Vurugu za kisiasa.
- Wananchi kuchanganyikiwa na kutokuwa na mwelekeo
- Imani kubwa sana katika Ulimwengu wa Roho
- Ujinga kwa kiasi kikubwa
Hata kama yapo basi ni kwa kiasi kidogo sana hivyo wananchi watakapoamua kurekebisha Msingi wao wa KIUCHUMI kwa aidha kufanya kazi au kuondoa unyonyaji basi hayo mambo yote yataisha (SIJUI KAMA NI KWELI)
NB 4: Mwisho kabisa,
Waafrika ni lazima tufike mahali tubadilike tena tusianzie kwenye ngazi za kisiasa kama ambavyo CHADEMA na CCM wanataka kutuaminisha uongo. Kabla ya mataifa kuzaliwa mwanadamu alianza kuwa na familia kwanza: Nadiriki kusema kwamba Familia Imara ndiyo msingi wa Taifa Imara. A Strong Family: The Foundation of A great nation. Mungu ana akili sana kuumba familia kabla ya Falme na mataifa makubwa.
Marekani na mataifa ya Ulaya yalikuwa na nguvu sana kwasababu ni watu wanojali familia kwa kiasi kikubwa sana. Mzazi anavyofanya kazi anakuwa na jambo moja tu kichwani "Maisha ya watoto wangu" Hivyo inapelekea mzazi kuhusika kwa namna moja au nyingine katika maendeleo ya mtoto kwa kiasi kikubwa.
Ukishambulia familia basi umeharibu taifa, naomba niwape ushahidi wa kihistoria katika hili:
- Adolf Hitler alivyokuwa tu Raisi wa nchi alifanya kitu kimoja kikubwa kwanza: Kugawanya familia na kupandikiza mambo yake. Alichoma vitabu vyote vya shule na kuanza kupandikiza sera za kinazi kwenye akili za watoto. Alitumia majasusi wa kike kupeleka taarifa kuhusu waume zao kama wanampinga na wanaume wengi sana Ujerumani walikufa kutokana na wake zao kupeleka taarifa kwa SS of the Third Reich.
- Mao Tse Tung alivyopindua Uchina kwenye Cultural Revolution alianza na watoto na kusema kwamba hawa ni mali ya taifa na watoto walichukuliwa na kupangishwa mstari na kuanza kuwatemea mate wazazi wao na kuwapiga kisa wao ni mapebari na adui wa Ujamaa. Hivyo baada ya kupandikiza sera za kikomunisti kwenye akili za watoto yeye alifanikiwa sana.
- Marekani ilianza kushambuliwa na sera mbovu na za hovyo kama Feminism na Homosexuality. Leo hii taifa la Marekani linaongoza kwa kuwa na taraka kwa zaidi ya Asilimia 50% ya walioona: Kuna siku nilikuwa nasikiliza ushahidi wa mpiga picha moja maarufu sana jimboni Texas, alisema huwa anapiga picha nyingi kwenye harusi lakini asilimia kubwa ya wateja wake anapowapelekea picha anakuta tayari wanakuwa wameshaachana. Katika hali hii watoto wanakuwa kwenye hali gani labda ??? Kulelewa na mzazi moja ni changamoto sanaaa, labda iwe tu ni mipango ya Mungu kama Ujane au Ugani. Lakini haya ya kujitakia tu kushika mimba au Kuzalisha na kusema ntalea tu ni mbinu za shetani ambazo zinatufaya tutingwe na mambo yetu na kusahau majukumu yetu ya msingi kama Uzazi. Taraka ni mchakato mrefu unaochanganya kichwa na kuleta umasikini sana hivyo mtu anajikita huko na anasahau mambo ya muhimu.