Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
MTOTO Bahati Mlelwa (3) amenusurika kifo baada ya baba yake mzazi kumjeruhi shingoni kwa kisu na kuutelekeza mwili wake kichakani.
Baba huyo, Halfan Mlelwa(28) mkazi wa kijiji cha Mnyagala katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amethibitisha unyama huu na kusema mtuhumiwa anahusishwa pia na mauaji mengine ya kutumia mapanga maeneo mengine.
Alisema tukio hilo lilifanywa juzi saa 11:00 jioni kijiji cha Mnyagala wilaya ya Tanganyika. Ambapo baba huyo alimtelekeza akijua ameua. Akisimulia alisema mtuhumiwa aliachana na mke wake akiwa na ujauzito wa mtoto Bahati.
‘’Jioni ya siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alifika kwa mke wake wa zamani ambaye hakuwepo akamchukua mtoto Bahati na kutokomea naye kichakani jirani na nyumba aliyokuwa akiishi mtoto huyo na mama yake akamuue,”alieleza.
Mtuhumiwa akiwa na mwanawe kichakani alichomoa kisu kibindoni akaanza kumchinja na kuondoka akiamini amemchinja na kumuua.
Inadaiwa mama wa mtoto huyo aliporejea nyumbani hakumwona mwanaye hivyo akaanza kumtafuta na kumkuta akiwa amezimia huku mwili mzima ukiwa umetapakaa damu.
Kamanda Kuzaga alisema opereshini ya jeshi la polisi inayoendelea wilayani humo dhidi ya watuhumiwa wa mauaji na uhalifu mwingine ilifanikisha kumnasa mtuhumiwa huyo haraka.
Alisema haijafahamika chanzo cha baba huyo kumfanyia unyama huo mwanaye ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi iliyopo mjini Mpanda kwa matibabu.
CHANZO: HABARILEO