Beira Boy
JF-Expert Member
- Aug 7, 2016
- 23,961
- 42,166
Aman iwe watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Geita, imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela, Imani Salehe (23) baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Hukumu hiyo imetolewa Aprili 30, 2025 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Calvin Mhina, baada ya mshtakiwa kukiri kosa la kumuua mtoto wake Monica Imani, bila kukusudia.
Kesi hiyo iliwasilishwa kwa ajili ya kusomewa hoja za awali, lakini Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Kabula Benjamin ameiomba Mahakama kubadilisha hati ya mashitaka kutoka kuua kwa kukusudia na kuwa kuua bila kukusudia, kinyume na Kifungu cha 195 na 198 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Akiwasilisha maelezo ya kosa, Wakili Kabula amesema tukio hilo lilitokea Septemba 17, 2024 huko Chato, mkoani Geita, Salehe alimuua mtoto wake Monica kwa kumyonga shingoni, kwa madai kwamba mtoto huyo alikuwa amechelewa kutembea, jambo lililomkwaza baba yake.