Baba alivyokuwa hai

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
4,393
7,043
Sisi tumezaliwa na baba mmoja ila watoto tupo milioni kadhaa!baba alivyokuwa hai alituaminisha kwamba sisi watoto wake tuna maisha mazuri sana na sisi ndio watoto pekee tunaishi vizuri ndio maana tunachukiwa sana na majirani hapa mtaani kwa hivyo tusiogope tujivunie kwa hilo!na sisi kama watoto tulimuunga baba yetu mkono kwa sababu ya ukali wake tulikubali kutangaza kwa majirani zetu kuwa tunaishi maisha mazuri pale nyumbani kwetu japo tulikuwa tunakula mlo mmoja tu kwa siku huku kila kukicha hali ikizidi kuwa mbaya lakini tuliendelea kulinda heshima ya baba yetu kipenzi huku mama yetu pia akimuunga mkono baba kuwa tuna baba imara sana, tulikubaliana na hali halisi jinsi ilivyo hata majirani wakitukaribisha chakula tulikuwa tunasema tumeshiba kweli kweli lkn ukweli tulikuwa tunaujua sisi watoto njaa ilikuwa ni kali sana ila tulimuogopa sana baba.

Ila baada ya baba kufariki mama ameanza kutupatia elimu mpya kwamba mficha maradhi kifo umuumbua kwa hivyo hali nyumbani kwetu ilikuwa ni mbaya sana japo tusimseme baba vibaya ila tukubali kwamba tulipitia kipindi kigumu sana japo baba alisema tulikuwa vizuri sana!

Mama ametusihi kwamba ni wakati wa kuamka kutoka usingizi na kujipanga upya kwani hatujachelewa sana!

Asante sana mama maana kabla ya 40 umeonyesha nia nzuri kwa sisi watoto wako wapendwa kwamba kuna tumaini jipya baada ya baba yetu kutangulia mbele za haki!

Asante sana mama tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu dhamira yako iwe ya kweli maana wanao tunakutegemea maana umri wetu bado mdogo sana kujitegemea
 
Tundu Lissu amewaomba msisifie sana kwanza, subirini hadi kuleeeee mwishoni ndio mtaamua ama msifie au mmponde
 
Majitu yanasema nchi ni tajiri ..

Kumbe wanajilipa posho na mishahara minono huku wananchi wanakula barabara na madaraja ....huku wakishindia mulo mmoja ...


Nchi ni masikini tu ...

Mama samia okoa nchii hii ,hakuna haja ya kujitenga na mataifa mengine vutia wawekazaji waje ajira zirudi ..
 
Majitu yanasema nchi ni tajiri ..

Kumbe wanajilipa posho na mishahara minono huku wananchi wanakula barabara na madaraja ....huku wakishindia mulo mmoja ...


Nchi ni masikini tu ...

Mama samia okoa nchii hii ,hakuna haja ya kujitenga na mataifa mengine vutia wawekazaji waje ajira zirudi ..
walichonikera chini ya daraja la mfugale wamezuia watu kulala
 
Kuna taasisi imekaa vikao kibao ndani ya mwaka mmoja na imejilipa pesa nyingi sana, lakini matokeo hakuna...

Awamu ya tano sijui ilikua wapi kutumbua watu kama hawa...
 
Baba alijua ipo siku utakua na hayo yote utayangamua mwisho wa safari yako ya mafanikio

Uwezi kuishi maisha ya mwenzako huo ni utumwa ishi maisha yako utakuwa huru moyoni mwako
 
Majitu yanasema nchi ni tajiri ..

Kumbe wanajilipa posho na mishahara minono huku wananchi wanakula barabara na madaraja ....huku wakishindia mulo mmoja ...


Nchi ni masikini tu ...

Mama samia okoa nchii hii ,hakuna haja ya kujitenga na mataifa mengine vutia wawekazaji waje ajira zirudi ..
Wale waliojilipa Mill 600
 
Back
Top Bottom