Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie Waandamana kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar Makonda

galindas

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
978
1,305
Baadhi ya wasanii wameandamana wakitokea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar kuelekea Kariakoo kwa lengo la kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje.

Wadau kwa uelewa wangu naona hili si sawa. Wasanii wa Bongo movie wanatakiwa kufanya kazi nzuri zitakazoteka soko la ndani na si kulazimisha watu wote tuangalie filamu zao hata zile zisizo na ubora.

Kazi nzuri inajiuza, kila mwenye kuzalisha bidhaa fulani akiandamana kupinga bidhaa zingine zisiingizwe nchini itakuwaje.

Nawakilisha.

fb_img_1492601541428-jpg.498250
fb_img_1492601648796-jpg.498253
 
Baadhi ya wasanii wameandamana wakitokea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar kuelekea Kariakoo kwa lengo la kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje.

Wadau kwa uelewa wangu naona hili si sawa. Wasanii wa Bongo movie wanatakiwa kufanya kazi nzuri zitakazoteka soko la ndani na si kulazimisha watu wote tuangalie filamu zao hata zile zisizo na ubora.

Kazi nzuri inajiuza, kila mwenye kuzalisha bidhaa fulani akiandamana kupinga bidhaa zingine zisiingizwe nchini itakuwaje.

Nawakilisha.

Mkulu ameshasema kwamba sasa hivi hakuna kupangiana bana!! Kwa nini watupangie cha kununua na kuangalia.. Wasanii tuheshimiane [HASHTAG]#TusipangianeChaKuangalia[/HASHTAG] jitahidini kutoa kazi nzuri watu watanunua tu, movie trailer dakika 30, poor quality hakuna hata balance ya sauti pindi waigizaji wanapoongea vs nyimbo za usindikizaji.. Mnataka tuangalie manini haya... acheni tuapate HD toka nje msituongezeee stress.
 
Asante wana Jf.
Kwa namna ya pekee niwapongeze sana wasanii wote wa Bongo movie Tanzania .
Lakini kwa upendo wa pekee nitumie ukurasa huu kumkumbuka marehemu Steven Kanumba(Ancle-JJ)kwa yale aliyoyafanya kwa muda mfupi alioishi duniani
hapa nakumbuka falsa ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema “ Ni bora kuishi maisha mafupi ya simba nyikani kuliko kuishi maisha marefu ya kondoo mwituni”

Sanaa hii ya maigizo ni kazi kama kazi nyingine wala kazi nyingine si bora kuliko sanaa hii, Kama wewe ni Rais,Waziri,Mbunge,RC, DC,DED, Meneja,Afisa ,Mkulima,Mfanyabiashara kamwe hupashwi kudharau wala kuladhalilisha wala kuzitumia vibaya kazi halali za kada hii.

Niwape pole sana Wasanii wa mbongo movie kwani taaluma yenu hapa Tanzania haiheshimiki wala kufikirika kwa Watawala hasa hawa wa awamu ya Tano, Ni majuzi tu Mkuu wa mkoa wa Dar-es saalam
Mh Paul Christian Makonda amekaririwa akiwasimamisha kama vikaragosi mbele ya Watanzani , Makonda alionekana kana kwamba anataka kuwasaidia ili hali shida yake ilikuwa ni kujitafutia vijiheshima kwa Mkuu wa inchi.

B-movie jiulizeni hivi ni kwanini mmefilisika kwa kiwango hiki, Hivi ni kwanini copy zenu hazinunuliki tena Sokoni!
B-movie jiulizeni kwanini umaarufu wenu umeshuka gafla? Jiulizeni kwanini wenzenu wa Bongo flava bado wako sokoni,
B-movie jiulizeni kwanini hampati coverage kwenye Matangazo ya biashara exclusive Majuto & Joti & Ray.

Sikilizeni kwa makini wana B- movie wetu mmekosea hapa;
B-movie wengi wenu mmejiingiza kwenye siasa kitu ambacho kimewapunguzia mashabiki, Kumbukeni siasa ni kama dini/timu za michezo,
B-movie mmewahi kujiuliza , Tangu lini mashabiki wa yanga wamewahi kununu jezi za simba!
B-movie mmewahi kujiuliza ,Tangu lini mashabiki wa Arsenal wamewahi kuipromoti Man united!
B-movie mmewahi kujiuliza,Tangu lini shehe akanunua Biblia !
B-movie tangu lini mwana-UKAWA anunue kadi za CCM!

Najua wengi wenu ni wanachama wa CCM,Nakimsingi ni haki yenu ya kikatiba,Mkumbuke pia kwa kufanya hivyo mmekubali kupoteza wafuasi wote wa UKAWA ambao wengi wao ni vijana (Teens-washikaji) ambao ndio wapenzi wa hizi movie zenu.
Mmeamua kuwekeza kwa wana-CCM ambao wengi wao ni mambumbu/hawajasoma pamoja na wazee ambao wengi wao wanawaona ninyi kama watu msiokuwa na maadili na ni malaya tu.

Makonda anawadhalilisha kuwa ninyi ni choka mbaya eti watu wanadurufu kazi zenu nasema HAPANA, Watu hawana tena haiba nanyi, Watanzania wanamchukia Makonda pamoja na ninyi kwa sasa,

Steve-Nyerere ameona kitu hiki ndio maana ameacha kabisa kuambatana na Makonda.
B-movie mnafahamu gharama za rebranding , B-movie mnajua mkipotea mtapotea jumla!
B-movie lazima mtazame niwapi ziliko fulsa zenu kwa sasa, B-movie fursa pekee mlionayo ninyi nikucheza na (peer) age.
B-movie tambueni haiwezekani mashabiki wenu niwapenzi wa Arsenal ninyi mnawaonesha hadharani hamko nao bali ninyi mko Man-U kamwe hamtafika mkiwa pamoja.

Achaneni na siasa uchwara hizi za Tanzania chungeni career zenu kwa manufaa yenu na familia zenu .
Hata kama Makonda atazuia CD toka inje bado ninyi hamtauza tu badilikeni katika kuishi na kaufanya kazi zenu hamuwezi kulazimisha soko kamwe, Wateja watanunua kile wanataka na wala sio kile anataka Magufuli wala Makonda.

Mwafwaaaaaaaaaaa.
 
Kwahyo kuwafuta wakorea kkoo ndio wanahis tutaangalia muvi zao? Akil zao wote sawa tu hao wanaoandaman

Halafu hivi mkuu wa mkoa wa huko Dar ana mamlaka gani ya kuzuia uingizwaji wa filamu nchini?

Au ndo mmeshaamua eti Dar ndo nchi. Sisi huku Kigoma tutaagiza kupitia Congo, Burundi, Rwanda na Uganda, nyie endeleeni kuhangaika na huyo jamaa yenu.
 
Baadhi ya wasanii wameandamana wakitokea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar kuelekea Kariakoo kwa lengo la kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje.

Wadau kwa uelewa wangu naona hili si sawa. Wasanii wa Bongo movie wanatakiwa kufanya kazi nzuri zitakazoteka soko la ndani na si kulazimisha watu wote tuangalie filamu zao hata zile zisizo na ubora.

Kazi nzuri inajiuza, kila mwenye kuzalisha bidhaa fulani akiandamana kupinga bidhaa zingine zisiingizwe nchini itakuwaje.

Nawakilisha.
Wapuuzi wanao sababisha biashara zao ziende ni haohao wa kariakoo 'They have to improve the qualities of their movies to beat competitions'
 
Siku ile Magufuli alipokua anazindua Hostel,nilona baadhi ya wasanii walikua wanampigia Bashite makofi nyuma yake,nilishajua lazima waje na drama.Siku haijapita nyingi drama tayari,Hiyo siyo kazi ya Bashite hiyo ni kazi ya Mwakyembe,Bashite wapi na wapi hapo?
 
Back
Top Bottom