Upo sahihi lakini pia wapo Wabulushi wa Iran. Wikipedia inasema:
Eneo la Balochistan limegawanyika kati ya nchi tatu: Iran, Afghanistan na Pakistani. Kiutawala inajumuisha jimbo la Pakistani la Balochistan, jimbo la Irani la Sistan na Baluchestan, na maeneo ya kusini ya Afghanistan, ambayo ni pamoja na mikoa ya Nimruz, Helmand na Kandahar .[5][6] Inapakana na eneo la Pashtunistan kaskazini, Sindh na Punjab mashariki, na maeneo ya Irani magharibi. Pwani yake ya kusini, ikiwa ni pamoja na Pwani ya Makran, inasogeshwa na Bahari ya Arabia, hasa sehemu yake ya magharibi, Ghuba ya Oman.
Chanzo:
Balochistan - Wikipedia
Kutokana na ramani niliyoipitia inaonesha Balochistan imetapakaa sana. Kihistoria wabulushi wametapakaa sana, wao ndiyo walikuja Afrika ya Mashariki na kuwatowa Wareno kwa nguvu, waliwatandika na kuwashinda Wareno licha ya kuwa wareno tayari walijichimbia kwenye ngome (fort Jesus) Mombasa na "Ngome Kuu" Unguja. Baada kuwatandika Wareno Waliikabidhi miji hiyo ya Mombasa na Unguja kwa watawala walioondolewa na Wareno.