Baadhi ya viongozi wa Saccos ya walimu wilayani Rorya watuhumiwa kuiba mil.600

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Baadhi ya viongozi wa Bodi ya Chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha walimu Saccos wilayani Rorya mkoani Mara,wanadaiwa kughushi majina ya walimu wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na kufanikiwa kuiba kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia sita zilizotolewa na benki ya CRDB kama mkopo wa kuwezesha ushirika huo kukopesha walimu wa wilaya ya Rorya.

Wakizungumza wakati Kaimu Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoani Mara akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa wizi huo,baadhi ya walimu ambao ni wanachama wa ushirika huo,pamoja na kuomba vyombo vya dola kuwakamata mara moja viongozi wanatuhumiwa kwa wizi huo mkubwa,lakini wamesikitishwa kuendelea kukatwa fedha kutoka katika mishahara yao katika kulipa deni hilo wakati hawajanufaika fedha hizo.

Naye Kaimu Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoani Mara bw Richard Majala, akitoa taarifa za ukaguzi huo,amesema tume iliyoundwa imethibitisha kuwa baadhi ya viongozi wa Bodi hiyo waliandikisha majina hewa ya walimu na wanafunzi na kufanikiwa kuiba fedha hizo,huku meneja uhusiano wa Benki ya CRDB Kanda ya ziwa na kati Bw Raymond Urasa,akitaka hatua kali zichukuliwe kwa wahusika katika kunusuru ushirika huo wenye lengo la kuinua hali za walimu wa wilaya ya Rorya.

Chanzo: ITV
 
Nashangaa walimu wanakatwaje deni kama hawajakopa? Hilo deni la CRDB si lingekipwa na wakopaji? Na kwa kuwa zimekwqpuliwa na wajanja si hao ndio wanaopaswa kulipa?
 
Nashangaa walimu wanakatwaje deni kama hawajakopa? Hilo deni la CRDB si lingekipwa na wakopaji? Na kwa kuwa zimekwqpuliwa na wajanja si hao ndio wanaopaswa kulipa?
Kutokujitambua!
 
Back
Top Bottom