Baadhi ya sifa za manabii wa uongo

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
3,832
Reaction score
4,425
Ni ngumu sana kuwatofautisha manabii WA UONGO na manabii WA KWELI mana hata shetani hujigeuza malaika na wote wanatumia jina la YESU na wanafanya miujiza kwa kutumia jina la YESU.

Mt 7:22
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

BAADHI YA SIFA ZA MANABII WA UONGO
1. NENO LA MUNGU.
Kati kati ya mahubiri yake atakuchanganyia na mafundisho ambayo yapo kinyume na NENO LA Mungu la BIBLIA(ni muhimu kulijua NENO/Biblia na kulifuata NENO linavyosema sio mahubiri ya mwanadamu,SHIKA NENO/BIBLIA.

2. KUMTUMAINIA na KUMTEGEMEA YESU...nabii WA Kweli ,lazima atakujengea Imani Yako umtegemee Yesu,napenda kumnukuu mch Laizer (RIP) mikutano yake alikuwa anapenda kusema,usiseme ni Laizer ameniponya sema ni YESU amekuponya sio Mimi Laizer,pia alikuwa anasema wote tumekutana hapa ni watumishi WA Mungu hata Mimi alikuwa anajiita mtumishi WA Mungu,akawa anasema wote sasa tuombe kwa YESU kila MTU aombe mana wote tumekuja kumuomba yeye na sisi wote ni watumishi WA Mungu.
Mtumishi WA Mungu WA KWELI atakuelekeza kwa YESU ,utukufu na heshima na SIFA atavielekeza kwa YESU.

NABII WA UONGO atakuelekeza kwenye utegemezi WA vitu(kama mafuta ya upako,maji ya upako,udongo WA upako)..au umtegemee yeye Yani ANACHUKua nafasi ya Yesu yeye au anakuelekeza utegemezi kwenye vitu VYA upako


3. MAOMBI YA KULIPIA
Mathayo 10:8
Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure.Maombi ya KULIPIA maombi ya laki moja...n.k

4. ATAKUWA RAFIKI WA WENYE DHAMBI NA HATAKEMEA DHAMBI NA ATAHALALISHA DHAMBI.
Vitu AMBAVYO ni dhambi yeye atasema sio dhambi(ulevi,suruali kwa wanawake,ndoa za jinsia moja n.k yeye atasema sio dhambi,atavitolea ufafanuzi wake WA kutetea dhambi,MATENDO yake anaweza akawa mzinzi,muongozo,mfitini, masengenyo,mlevi n.k

Lakini atapendwa na wenye dhambi,injili ya KWELI inachoma UKWELI unauma,unaona manabii WA KWELI WA biblia walichukiwa na wafalme wenye dhambi,walikamatwa na kuweka magerezani,wengine walikatwa vichwa kwa kukemea movu..

6. ATAKUWA NA PEPO LA UTAMBUZI.
atakutabiria umezaliwa LINI,unaendelea kunywa soda gani.mana anakuwa na pepo la utambuzi , sasa YESU hawezi kumtuma Nabii akutabirie unakunywaga soda Gani unayoipendelea..usishangae vitu vyote anavyokutabiria vingi vitakuwa vya KWELI.(pepo la utambuzi)..lakini anaweza akawa MFARAKANISHI akakufarakanisha na ndugu zako,atakwambia ndugu Yako fulani mfano mama mkwe WAKO ndiye mbaya WAKO(anatengeneza uadui KUVUNJA familia,KUVUNJA UMOJA na maelewano)
Mt 5:9
Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Hata kama ni KWELI mama mkwe WAKO ndiye anayetumiwa na shetani kukufanya UBAYA,bado hatakiwi kukwambia mama mkwe WAKO ndiyo mbaya WAKO.
mana hapo ADUI YENU ni SHETANI,siyo uadui wa wanafamilia kuwachonganisha ndugu badala kuwapatanisha.
usipende kutaburiwa tabiriwa na mitume na manabii.

7. ANAWEZA KUNENA KWA LUGHA
lugha ya kuzimu nayo inafanana kwa KIASI na lugha za malaika,kwa sababu shetani naye kabla hajawa shetani alikuwaga malaika,na alipotupwa DUNIANI,hakunyang'anywa uwezo baadhi,hasa WA kudanganya watu,(ni baba WA UONGO) ni HILA zake.
 
Umesema vema.Lakini hebu tujiulize,hivi hawa manabii wanajitambua kwamba.

Wanatumika na mwovu shetani?Hawa jamaa wamefumbwa macho ya kiroho wasitambue kuwa wanamtumikia shetani.Kwa sababu wanatumia jina la Yesu katika maombi na wakati mwingine wanahubiri vizuri.Tutafanya makosa tukiwalaumu badala yake Mungu awatokee kama alivyomtokea sauli wapate kumtumikia yeye badala ya ibilisi
 

Manabii WA UONGO wengi wao walianza kwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI, mwanzoni wengi wao waliitwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI,ila KATIKATI ya safari Yao wakabadilika na kuanza KUMTUMIKIA SHETANI kwa sababu mbali mbali,mana shetani pia anawa ahidi ana wavutia kwa mali mafanikio ya DUNIANI.Ni wachache sana ambao toka mwanzo walianza wakijua kuwa watakuwa manabii WA UONGO ila wengi walianza na Mungu(Rohoni) wakamalizia mwilini wakakengeuka wakaasi,wakifikiri wamesimama wakaja wakaangukia kumtumikia SHETANI.
Ukiwaombea wanaweza wakavunja maagano na kuzimu wakatoka...sema inakuwa ni ngumu kuwatoa HUKO kwa sababu wame asi wakiwa wanajua DHAMBI ZA MAKUSUDI WAMEASI..

ila KWA MUNGU yote yanawezekana yasiyowezekana kwa mwanadamu.

Mungu awaokoe manabii WA UONGO.
 
8.8.Manabii WA UONGO wengi wao mwanzoni walianza kwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI, mwanzoni wengi wao waliitwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI,ila KATIKATI ya safari Yao wakabadilika na kuanza KUMTUMIKIA SHETANI kwa sababu mbali mbali,mana shetani pia anawa ahidi ana wavutia kwa mali mafanikio ya DUNIANI.Ni wachache sana ambao toka mwanzo walianza wakijua kuwa watakuwa manabii WA UONGO ila wengi walianza na Mungu(Rohoni) wakamalizia mwilini wakakengeuka wakaasi,wakifikiri wamesimama wakaja wakaangukia kumtumikia SHETANI.
Ukiwaombea wanaweza wakavunja maagano na kuzimu wakatoka...sema inakuwa ni ngumu kuwatoa HUKO kwa sababu wame asi wakiwa wanajua DHAMBI ZA MAKUSUDI WAMEASI..

ila KWA MUNGU yote yanawezekana yasiyowezekana kwa mwanadamu.

Mungu awaokoe manabii WA UONGO.
Tuwaombee manabii WA UONGO waokoke waache kutumika na ADUI.
AMEN.🙏🏿
 
9.Sifa nyingine ya manabii WA UONGO ,watahubiri INJILI YA MAFANIKIO MUDA WOTE prosperity gospel na KWAMBA kuwa MLOKOLE ama MKRISTO ni lazima uwe TAJIRI ni lazima uwe na afya njema wakati wote.

ANGALIZO usininukuu vibaya sio kwamba natetea UMASIKINI ama napenda umasikini ama namaanisha wakristo wawe MASIKINI.

POINT iliyopo KUMUHAKISHIA MLOKOLE ama MKRISTO ni lazima awe na UTAJIRI NA MAFANIKIO YA MWILINI kwa sababu ameokoka ,ni UONGO siyo sahihi Wala sio LENGO kuu la wokovu,Wala Yesu hajawahi kutuhakikishia kuwa tukimfuata Yesu atatufanya matajiri HAPA DUNIANI mafanikio ya KIMWILI.

Timoteo 2:312
Na wote wapendao kuishi maisha ya UTAKATIFU/UTAUWA katika KRISTO YESU ,WATATESWA

na tumeona watakatifu wengi WA mwanzo waliteswa.
ama wengine waliugua magonjwa na wengine walikufa kabisa kwa magonjwa mabaya makali kama Nabii ELISHA japo hata baada ya kufa mifupa yake ilifufua maiti ya MTU(pamoja na kwamba Nabii ELISHA aliugua UGONJWA mbaya akafa bado mifupa yake ilikuwa na upako na nguvu ya Mungu ya KUFUFUA maiti ya MTU)

Na hata wale waliokuwa matajiri(IBRAHIMU,AYUBU),walipitia pia MAJARIBU...IMANI YAO Ilijaribiwa.
Ibrahimu---amepitia MAJARIBU mengi ya kumpima Imani,hata Ayubu n.k

9.HAWATAHUBIRI UTAKATIFU..WATU WAACHE DHAMBI
watafundisha kuwa huwezi kuwa mtakatifu DUNIANI.
Ila maandiko yanasema
Utakuwa mtakatifu DUNIANI Zaburi ya DAUDI , inasema watakatifu waliopo duniani ndio Mungu hupendezwa nao.

Watafundisha UTAKATIFU utaupata utakapokufa UKIFIKA MBINGUNI sio kwenye maisha haya ya sasa mana kwa maisha ya sasa hakuna uwezekano WA kuwa mtakatifu kwa kipindi HIKI labda enzi za ZAMANI , kizazi hiki haiwezekani.

Biblia INASEMA tutakuwa watakatifu katika ulimwengu huu huu WA sasa TITO 2:11-12

Ukweli ni kwamba baada ya kufa hapa duniani ukiwa katika dhambi huwezi kutubu baada ya kufa au watu wakuombee uende peponi kama WEWE mwenyewe haukuishi maisha ya UTAUWA UTAKATIFU kipindi ungali hai kabla hujafa,baada ya kufa kinachofuata ni HUKUMU kutoa hesabu ya MATENDO yako,na kuvuna ulichopanda ukiwa kipindi ukiwa hai duniani,UNAOKOA DUNIANI SIO MBINGUNI.

10.BAADHI YA MANENO YA BIBLIA WATAYAKATAA YANAYOWACHOMA EATAJARIBU KUYABADILISHA KUYATAFSIRI UPYA VIBAYA WATASEMA HAYATUHUSU SISI HATUKUANDIKIWA HAYA SISI WALIANDIKIWA BARUA WENGINE..Tena haikuwa na MAANA hiyo watatoa maana FEKI ili KUHALALISHA DHAMBI WANAZOZIPENDA.
Watataka Mungu atubariki kwa baraka za IBRAHIMU WA agano la kale lakini baadhi ya MAANDIKO ya agano la kale watayakataa yale wasiyoyapenda wao.

Vitabu hivyo hivyo vya PAULO watasema ni barua TU kwa makanisa mengine Tena kwa WAKATI ULE sio wakati huu
ILA katika barua hizohizo za Paulo wakikuta mistari ya BARAKA na USHINDI WA vita vya kiroho itakayokurahisha wakaipenda WATASEMA hii SAWA tumeandikiwa sisi..ila katikati ya barua za PAULO wakikutana na MAONYO yanayowakemea waache dhambi MAKATAZO ..watayakataa watasema hii siyo ya kwetu haya wameandikiwa WAKIRINTHO sisi sio wakorintho..
hasa kwenye mambo ya mapambo,vitu bandia mapambo ya wanawake na manywele kusuka suka n.k
WATASEMA hiyo haituhusu ni ya wakorintho ila kama kuna andiko linalowafurahisha la wakorintho watalidandia kuwa ni LAO PIA.

MANA katika biblia yote SISI NI KINA NANI SASA mana kama SISI sio Wakorintho,SAWA kwenye biblia hii TUNAYOITUMIA SASA HIVI sisi ni kina nani sasa humo ndani?tulichoandikiwa sisi specifically Cha kwetu peke yetu ni kipi sasa?
Na kama barua za Paulo hazituhusu sisi kwanini waliziacha hawakuziondoa wakawapelekea wenyewe wakorintho sisi wakatuachia maneno yanayotuhusu sisi TU?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…