Baadhi ya mission za CIA usizozijua

Baadhi ya mission za CIA usizozijua

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,564
Reaction score
7,324
Wakati wa Vita Baridi, yaani Cold War, vita ambavyo vilikuwa kati ya Marekani na Urusi, bila kutumia bunduki, Marekani waliamua kutumia wanyama na ndege kama wapelelezi wao.

Walimchukua paka, wakamuwekea microphone ili aende kupeleleza Urusi. Kwenye mission yake ya kwanza tu, kwa bahati mbaya huyo paka akagongwa na gari, akafariki dunia.

Hawakuishia hapo, pia waliwapa mafunzo njiwa kwa ajili ya kwenda kupiga picha huko Urusi. Njiwa hao walikuwa wakitumika kama zinavyotumika drones leo hii.

Pia Marekani wakamtumia vampaya feki kwenye mission zao huko Ufilipino. Walimchukua jamaa, wakamuwekea meno, wakachukua maiti kadhaa, wakazilowanisha damu halafu naye jamaa wakamuwekea damu. Hilolikawaogoepesha waasi nchini humo na kutokomea kwa kuhisi sasa mavampaya yameingia nchini humo.

Pia CIA walitumia filamu kwenye mission zao mbalimbali, pia kwa kutumia muvi za Kimarekani, walizitumia kwa ajili ya kuwawafanya Iran kuwaachia mateka wao mwaka 1979. Ilikuwaje? Kaiangalie filamu iitwayo Argo. Wewe unaangalia filamu kama Commando ya Arnold Schwerzenegger, unaangalia filamu kama Rambo, Filamu za Commando Kipensi, Predator, Delta Force ya Chuck Norris, Black Hawk Down, Navy Seal, na nyinginezo za kivita au za kijeshi unashangaa.... wenzako pale ndio wanaeneza propaganda zao kuhusu nguvu na ujuzi wa kijeshi, na Jambazi kuu lazima awe Mwarabu, muafrika, Mrusi, Mmexico, au mtu yeyote aliye nje ya mfumo wao wa kiutawala... Kazi nyingine ya Hollywood ndio hiyo ya kueneza nguvu na propaganda za Mmarekani kupitia Filamu.

Pia kwenye mission zao walitumia bastola ya siri ambayo ilikuwa ikimsababishia mtu atakayepigwa nayo matatizo ya moyo na kufariki dunia ndani ya dakika chache. Hii waliitumia sana kwa watu waliotaka kuwamaliza, ukipigwa, utakufa na hata mwili wako ukichunguzwa, kitu pekee watakachogundua ni kwamba ulikuwa na matatizo ya moyo.

Kwa kifupi ukifuatilia mbinu za hawa CIA wanazotumia kumshinda adui utashangaa, ni kama zile mbinu alizofanyiwa Idd Amini na jeshi la Tanzania mpaka akaamua kukimbia nchi akijua ni Makomando Maalum wanaingia kumbe ni Wakurya kutoka Tarime wamebeba mapanga na kupewa kozi ya ukakamavu ya miezi 2 na kupelekwa vitani kagera.

Yani unaweza kujiuliza Marekani anashindaje mambo mengi na kusimika nguvu, kumbe ni movie na propaganda za uongo za kuwaogopesha maadui ambao wanajaribu kuwa tishio kwake. Ukipigwa Mwala mmoja na Marekani lazima ufyate mkia kwa sababu tayari kupitia fikra na mawazo ya vitu unavyosikiliza na kuvitazama maishani mwako wameshakutengeneza uwaogope.
 
Back
Top Bottom