BAADHI YA MASWALI UNAYOJIULIZA KATIKA SOKA.

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
**Mwanzilishi wa mpira wa miguu (Modern Football) unaochezwa leo duniani ni nani?

Ebenezer Cobb Morley alizaliwa tarehe 16 Agosti 1831 na alifariki dunia tarehe 20 Novemba 1924.
Anajulikana kama "Father of Association/Modern football".. Ni mwanamichezo wa Kiingereza.
Morley alikuwa katibu mtendaji wa kwanza wa chama cha mpira England FA 1863-1866 pia alichaguliwa kuwa rais wa pili wa FA 1867-1874.
Akiwa nyumbani kwake Barnes alitengeneza draft ya kwanza ya sheria 17 za mpira wa miguu zinazojulikana kama 17 laws of the game.

**Klabu gani ya soka ni kongwe kuliko zote?

Sheffield Football Club ya Uingereza ndio klabu ya mpira wa miguu kongwe kuliko zote inayotambuliwa na FA na FIFA.
Ilianzishwa tarehe 14 Oktoba 1857.

**Gianni Infantino ni Rais wa ngapi wa FIFA na waliomtangulia ni yapi majina yao?

Gianni Infantino ni Rais kudumu wa 9 wa FIFA na ametanguliwa na marais 8 kabla yake huku Mfaransa Robert Guerin akiwa binadamu wa kwanza kuongoza shirikisho hilo linaloongoza soka duniani.
Hii ni full list ya marais wa FIFA tangu kuanzishwa kwake.

01.Robert Guerin 1904-1906 (France)

02.Daniel Burley Woolfall 1906-1908 (U.K)

03.Jules Rimet 1908-21 (France)

04.Rodolphe William Seeldrayers 1921-1954 (Belgium)

05.Arthur Drewry 1956-1961 (U.K)

06.Sir Stanley Rous 1961-74 (U.K)

07.Joao Havelange 1974-98 (Brazil)

08.Joseph S Blatter 1998-2015 (Switzerland)

09.Gianni Infantino 2015-present (Swiss-Italy)

**Je ni kweli kwamba FA ni chama cha soka kikongwe zaidi ya FIFA?

Ni kweli kwamba FA ndicho chama cha soka kikongwe kuliko vyote juu ya sayari,kilianzishwa rasmi tarehe 26 Oktoba 1863,,kiumri FA imeizidi FIFA miaka 40 kwani FIFA ilianzishwa rasmi tarehe 21 mei 1904.

**Kwanini Taifa la Brazil ni mahiri katika soka?

Itakuwa ni dhambi ya karne kama ukifikiria kuhusu soka na usiione picha ya wabrazil wenye mpira wao.

Mabingwa Mara tano wa dunia,wachezaji walioacha alama katika soka,Pele,Ronaldinho,Zico,Garincha,Ronaldo,Rivaldo,Romario n.k.

Lakini wengi tunaweza kujiuliza ni kwanini wabrazil wana uwezo wa kipekee katika soka?

Hizi ni baadhi ya sababu

01.Futsal & Beach Soccer.
Hii ni aina ya michezo inayochezwa kwa kiasi kikubwa sana nchini Brazil.Pele anasema "Futsal makes you think fast and play fast,it makes everything easier when you later switch to football",, Futsal inachezwa katika uwanja mdogo na wachezaji watano kila upande,inasemwkana ni aina ya michezo migumu sana ukichanganya na Beach Soccer na wachezaji wengi wa Ki-brazil huanza kucheza kabla ya kuingua katika soka.
Futsal na Beach Soccer inasemekana ndio inayowapa uwezo mkubwa wachezaji wa ki-brazil kuwa wanyumbulifu,Kasi,Uwezo mkubwa kukokota mipira,umiliki na ubunifu mkubwa katika soka.

02.Winning Mentality
Wachezaji na mashabiki wa soka nchini Brazil hawaamini katika kushindwa,full stop!!,,Wachezaji hua wana matarajio makubwa zaidi katika soka,na hii inatokana na deni kubwa lililoachwa na waliopita,hakuna asiyelijua hilo kuhusu mafanikio ya Brazil katika soka.Hali hii huwafanya wachezaji wa kibrazil kujituma zaidi.

03.Ukubwa wa Brazil,Idadi ya watu na mpira ndio dini yao.
Huwez kuamini ila utaamini uingereza inaingia karibu Mara 33 ya ukubwa wa nchi ya Brazil,wazungu wanasema "Big is beautiful",Ukubwa wa nchi ni rasilimali tosha katika soka kama ikitumiwa vizuri.
Kama ulikua haujui 3% ya wanadamu wote ni wabrazil na mpira wa miguu ni mithiri ya dini nchini Brazil
Kwa idadi ya watu duniani Brazil inazidiwa na China,India,Indonesia & USA pekee.
idadi ya watu inaweza pia kuchagiza katika kutoa idadi kubwa ya vipaji.

****Haya ni baadhi ya maswali wanayojiuliza sana wanasoka.
 
Tunaomba next time tuletee jinsi soka lilvyoingia nchini kwetu, maana wengi no mashabiki tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom