BAADHI YA MAMBO YATAKAYOUA NDOA/UHUSIANO WAKO.

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
1. Utaua ndoa/uhusiano wako kama muda wote utakuwa mlalamikaji kwa mwenza wako na kutafuta mtu wa kumlaumu kila wakati. Huwezi kutatua tatizo kama huchukui hatua ya kuwajibika na badala yake ukawa mtu wa kulalama na kulaumu tu.

2. Utaua ndoa/uhusiano wako kama una tabia ya usumbufu endelevu. Usumbufu ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya anguko la ndoa nyingi.
3. Utaiua ndoa/uhusiano wako kama utatumia muda mwingi kwenye simu na kumpuuza mwenza wako.

4. Utaua ndoa/uhusiano wako kama utaruhusu wivu uliopindukia ukuendeshe. Wivu uliokithiri sio mzuri kwa ndoa na uhusiano, ni ugonjwa mbaya wenye madhara kwako binafsi na kwa ndoa yako kwa ujumla.

5. Utaiua ndoa/uhusiano wako ukiishi bila kazi na kuamua kuwa tegemezi wa kila kitu kwa mwenza wako, ukaacha kutafuta shughuli ya kufanya. Hakuna kinachoua ndoa haraka kama mwenza anayesubiri kufanyiwa kila kitu na kuwa tegemezi kwa kila jambo.

6. Utaiua ndoa/uhusiano wako kama utatawaliwa na chuki dhidi ya marafiki Pagdugu wa mwenza wako. Ukifanya hivyo, ndoa yako itakuwa hatarini. Sio lazima uwapende, lakini hutakiwi kuwachukia.
7. Utaua ndoa/uhusiano wako ukiamua kuishi na mwenzako kwa kuangalia historia yake badala ya kuangalia namna alivyo kwa sasa.

8. Utaiua ndoa/uhusiano wako ukiwa unamlinganisha mwenza wako na mpenzi wako wa zamani au mpenzi wa rafiki yako. Hutakiwi kumfanya mtu wa nje kuwa kipimo cha ndoa/uhusiano wako.

9. Utaiua ndoa/uhusiano wako ukiwa na kawaida ya kutotenga muda wa kukaa na mwenza wako. Unapofanya hivyo, unakuwa unamfundisha mwenzako kwamba anaweza kuishi bila wewe.

Wivu, hasira za kulopoka, kuongea bila uzipitisho na kua na ahadi zisizotekeleka ndoa yako itakufa ndani ya miezi minne tu
 
Haya mambo ya mahusiano hayana formula maana yanaongozwa na hisia. Usijifanye mjuaji saana wa mambo haya. Mwisho wa siku utachokwa na mada zako nyingi.

Sent using Infinix Hot 5
 
1. Utaua ndoa/uhusiano wako kama muda wote utakuwa mlalamikaji kwa mwenza wako na kutafuta mtu wa kumlaumu kila wakati. Huwezi kutatua tatizo kama huchukui hatua ya kuwajibika na badala yake ukawa mtu wa kulalama na kulaumu tu.

2. Utaua ndoa/uhusiano wako kama una tabia ya usumbufu endelevu. Usumbufu ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya anguko la ndoa nyingi.
3. Utaiua ndoa/uhusiano wako kama utatumia muda mwingi kwenye simu na kumpuuza mwenza wako.

4. Utaua ndoa/uhusiano wako kama utaruhusu wivu uliopindukia ukuendeshe. Wivu uliokithiri sio mzuri kwa ndoa na uhusiano, ni ugonjwa mbaya wenye madhara kwako binafsi na kwa ndoa yako kwa ujumla.

5. Utaiua ndoa/uhusiano wako ukiishi bila kazi na kuamua kuwa tegemezi wa kila kitu kwa mwenza wako, ukaacha kutafuta shughuli ya kufanya. Hakuna kinachoua ndoa haraka kama mwenza anayesubiri kufanyiwa kila kitu na kuwa tegemezi kwa kila jambo.

6. Utaiua ndoa/uhusiano wako kama utatawaliwa na chuki dhidi ya marafiki Pagdugu wa mwenza wako. Ukifanya hivyo, ndoa yako itakuwa hatarini. Sio lazima uwapende, lakini hutakiwi kuwachukia.
7. Utaua ndoa/uhusiano wako ukiamua kuishi na mwenzako kwa kuangalia historia yake badala ya kuangalia namna alivyo kwa sasa.

8. Utaiua ndoa/uhusiano wako ukiwa unamlinganisha mwenza wako na mpenzi wako wa zamani au mpenzi wa rafiki yako. Hutakiwi kumfanya mtu wa nje kuwa kipimo cha ndoa/uhusiano wako.

9. Utaiua ndoa/uhusiano wako ukiwa na kawaida ya kutotenga muda wa kukaa na mwenza wako. Unapofanya hivyo, unakuwa unamfundisha mwenzako kwamba anaweza kuishi bila wewe.

Wivu, hasira za kulopoka, kuongea bila uzipitisho na kua na ahadi zisizotekeleka ndoa yako itakufa ndani ya miezi minne tu
imara sana hii na kujiongeza pia muhimu
 
Back
Top Bottom