Mambo ya kutegana hayapo ,CCM kibao wataondoka mmoja mmoja ,wengi wameshajua kama kuna genge linawaburuza na baada ya kupita KATIBA watakuwa kama product ya chakula kilicholiwa.Na kubwa wataambiwa kwani zile laki tatu mlifikiria mnapendwa sana ?
Mtashangaa sana nyie mliekunywa maji ya bendera ,ila kama nijuavyo kuna CCM kibao hawakubaliani na kinachofanyika yaani kikinuka tu basi mabasi yakuwasafirisha wajumbe nje ya Dodoma yatakuwa hayatoshi.
Siku zote haki inakuja juu tu na wapenda amani na utulivu ni wale wanaopenda kuona haki inafanyiwa na kupewa haki yake hawako tayari kuona inakandamizwa ,tegemeo lao ambalo liliwafanya kubaki ni kuona labda kesho mambo yatakaa sawa ,labda rasimu ya Warioba itarudi mezani ,dalili zote za kurudi mezani kwa rasimi orijno hazipo hivyo hakuna kinachowafanya wabakie.