bunker burster
Member
- Jan 4, 2016
- 11
- 2
Wadau nawasalimu, poleni na majukumu
Kuna huyu msichana hapa kwenye shirika letu aliwahi kuwa mpenzi wangu yapata miaka 2 sasa, akarubuniwa na zee moja hivi lenye cheo na akaamua kuniacha, nikayapokea matokeo na ku move on
Tangu rais magufuli kuapishwa kumekua na kamata kamata ya viongozi wa mashirika ya umma, tumeshuhudia wengine wakikamatwa na wana usalama hapa hapa kazini kwa aibu kubwa, zee la huyu binti ni moja ya wahanga wa zoezi hili, mzee huyo yupo ndani kwa sasa uchunguzi ukiendelea, hali ya binti kiuchumi imezorota mno, sasa anakuja na hot pot la chakula kutoka nyumbani sababu ya ukata, tulizoea kumuona akienda luxurious restaurants
baada ya mfululizo wa majanga kumkumba, ikiwemo tatizo la kodi ktk apartment anayoishi, p kuuguliwa na mzazi, kushindwa ku graduate masters kutokana na kushindwa ku fulfill requirements, kuitwa na wana usalama na kuhojiwa kila mara, kana kwamba hiyo haitoshi kuna tetesi kuwa yumo kwenye orodha mpya ya wanaotarajiwa kusimamishwa kwa magumashi mbali mbali waliyoyafanya kwa kushirikiana na mabosi walio ndani kwa sasa
Ndipo baada ya haya yote, jumamosi narudi kwangu usiku namkuta huyu binti kwenye ngazi za nyumba yangu akiwa ananisubiri, mida ya saa tatu, nikamuuliza vipi kuna tatizo? Akaniambia anaomba kuhamia kwangu kwa muda hadi matatizo yake yatakapoisha, kwamba kwake sasa hivi kupo under 24 hrs surveillance na isitoshe kodi imeisha a week ago, hivyo wamemvumilia tu
Kwamba chonde chonde nisifikirie ya nyuma, kwamba wazazi wetu wanafaamina, kwamba sisi ni majirani kule kijijini, kwamba ndio maana hakuona mwingine wa kumsaidia, kwamba roho wa mungu amemuonesha mm ndie mwanaume sahihi kwake, na kwamba hatorudia makosa tena
Wadau sijui mlikua mnasemaje?