Mimi bado najiuliza ni "turning point" ipi iliyosababisha wana-UKAWA kutoka nje ya Bunge. Kama ni msimamo imara wa CCM juu ya Serikali 2 wana-UKAWA wanaufahamu tangu wanaripoti pale Bungeni na wanaonekana walikuwa ready kupigana mpaka mwisho!
Tunajua wana-UKAWA walijenga hoja kuwa Muungano huu hauna Hati na ni BATILI! Hoja hii iliwapa morali wa kusonga mbele, liwalo na liwe! Sote tulishuhudia matusi ya nguoni ya "Mwanasheria Nguli" Tundu Lissu dhidi ya Waasisi wa Muungano! Huu ujasiri aliokuwa nao Tundu Lissu umewashangaza wengi, mpaka mwasisi wa CHADEMA Mzee Mtei alipomkemea Tundu Lissu kwa kukosa hekima na adabu!
Mara tukamwona Mzee Stephen Wassira, almaarufu kama Tyson, akanyanyuka pale mjengoni hivi majuzi akijigamba kuwa atawasilisha Hati ya Muungano ndani ya Siku 2!
Hatua hiyo imebadili kabisa upepo wa UKAWA na tumeshuhudia wakijitoa mjengoni ili kwenda "kushtaki kwa wananchi!"
Bado sitaki kuamini kuwa ni ile Hati ya Muungano halisia iliyowatoa mjengoni lakini kuna mazingira yanayounganisha matukio hayo mawili!
Hii ni kwa sababu UKAWA walijua msimamo wa CCM ambao hakuna asiyefahamu kuwa JK aliusisitiza wakati wa Hotuba ya Kuzindua Bunge Maalum la Katiba! Kama hivyo ndivyo basi, WHY NOW?
TUJADILI!