Baada ya udini sasa mnaanza ukabila

Baada ya udini sasa mnaanza ukabila

Status
Not open for further replies.

hacena

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
617
Reaction score
208
Baada ya udini kuhubiriwa kwa muda mrefu na ccm, kuwa chadema ni chama cha wakristo na hoja hiyo kuishia kwa mbunge wa arusha mjini kumuita rais wa jamhuri kuwa muasisi wa udini, sasa ccm huko arusha wameanzisha ukabila. Eti kuanzia mwenyekiti wa mtaa na kuendelea wawe waarusha/wamasai.

Swali ni kuwa nani ni muarusha, mmasai, mchaga au kabila jingine? Mimi binafsi baba yangu na mama yangu waliamia arusha mwaka 1975, kama waajiriwa wa serekali, na walitumia nguvu zao kuijenga arusha baba yangu ni mstaafu sasa, nimezaliwa arusha na kukulia arusha, na sasa nafanya kazi kama muajiriwa wa serekali nje ya arusha sasa mimi nikizaa watoto huku nao wakibaguliwa waende wapi? Ni aibu kubwa kwa ccm kumuogopa lema kiasi kwamba wanaamua kupoteza kura zote za wachaga.

Majibu ya uchaguzi wameyaona na ni vyema kwa ccm kuacha siasa za maji taka.
 
Za j3 wakuu:

Pamoja na furaha niliyonayo toka jana,leo nina machache ya kuwashauri ccm,kuwa haya mambo ya kuhubiri ugaidi,udini,ukabila,upadre,usoweto,ukilolo,umorogoro,uigunga zimepitwa na wakati,kama nikujaribu basi majibu mshayapata<arusha> kuwa hizi sera za umimi haziuziki tena hapa Tanzania,kuua watu nakusingizia cdm wakati sote tunaona chanzo ni nini nalo halina nafasi tena,tengenezeni team yetu chini kwa chini,acheni tambo,acheni kutumia police kuangamizi upinzani,chekeni na adui zenu kama mlivyocheka na cuf na udp,tlp,na sasa nccr ila niwakumbushe tu kuwa cdm wako kazini,wako serious,wako tayari,wako makini,wameweza na sasa wanasonga mbele.


Tulizaliwa ccm,tukakulia ccm ila tumekataa kufia ccm,kwa sababu tunu za Taifa hili ccm hazitaki tena,haitusikilizi tena,imekumbatia matajiri na kusahau masikini,mda bado mnao,vichwa ccm bado vipo vingi tu,mawazo yakujenga ccm ya leo na kesho yapo,ila hamyataki,mnataka mawazo ya nape na mwigulu,hamuwezi kwenda popote,mkizembea mwisho wenu ni 2015.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom