Baada ya tarehe 25 October, Tusilaumiane!

Baada ya tarehe 25 October, Tusilaumiane!

Naanza kuwatahadharisha watanzania wote, baada ya uchaguzi mkuu tusilaumiane:

Nimeona wasanii sasa hivi wanajikomba CCM, baada ya uchaguzi ndio watagundua kwamba serikali bado haiwajali, Tusilaumiane!

Naona bado kuna wakinamama wenye shida za kutupwa, bado wanasema CCM ni nzuri, baada ya uchaguzi, ndio wataanza tena kulalamika, Tusilaumiane!

Naona kuna baadhi ya vijana wanapewa vifedha na kujisahau, baada ya uchaguzi, ndio watakumbuka kumbe hawana ajira, Tusilaumiane!

Naona watanzania wengi tumekuwa tukilalamika maisha magumu, baada ya uchaguzi, maisha yatabadilika kutokana na chaguo lako, ukichagua
CCM, Tusilaumiane!

Chagua mabadiliko, vinginevyo, TUSILAUMIANE!!!!

Wasanii wabongo ni wasanii kweli yaani vichwa tikiti maji utaona tu
 
Umeanadika maneno ya busara na hekima sana. Mimi nlishawambia ndugu zangu vijijini nkigundua unaishabikia ccm na kuipigia kura. Usinililie shida. Mfano lowasa kashasema atafanya awezalo elimu iwe bure mpaka chuo na matibabu apunguze gharama. Nimewambia ukichagua ccm na kilaza magufuli. Mtu asiniombe hela ya ada au michango ya madawati.

Uko sahihi, Mi sina bajeti ya ada ya mtu yeyote zaidi ya mahitaji ya wanangu pekee.

Anaependa kulipia ada na michango achague CCM na asiyependa achague CHADEMA. hivyo kila mtu abebe mzigo kadri ya uchaguzi wake
 
Mimi mmoja wa wanaoichukia ccm kuzidi chochote duniani, lakini kubadili ccm kwa ajili ya lowassa, hilo sikuabaliani hata kiama, bora ccm warudi tu,
Wapuuzi kina mbowe wametuuza mwaka huu tungeshinda kwa nguvu zetu bila kuazima hiyo mizoga ya ccm isiyo na usafi wala uadilifu, eti Leo ndio imekuwa tumaini letu, ujinga kabisa, mbwa waliotukamua miaka mbwa waliotutafuna miaka leo ndio walinzi wa mageti yetu, upumbavu kabisa

Kwanza kabisa Lowassa hashindi urais hiyo sasa ni dhahiri hata mtoa mada anaonekana kuanza kukubali matokeo na kuanza kulalama eti ooh tusilaumiane. Nani atamlaumu? Kwi kwi kwi
Pili kama uko radhi kura yako ipotee, mi nitampa Anna Mghwira au Hashim Rungwe lakini siyo Lowassa who is not the change we want but more of the same!
Wanamabdiliko wa kweli tumwachie Magufuli tuone kama kutakuwa na mabadiliko navtujipange upya!
 
MABADILIKO gani CCM wanaweza kuleta nchi imesheni rasilimali lakini CCM miaka 54 ni zero hakuna hata sector moja inayofanya kazi zote ni zero. elimu=0 Maji=0 umeme= 0 miundombinu=o kilimo=0 afya=o
 
Back
Top Bottom